AJALI MBAYA YATOKEA CHANG’OMBE JIJINI DAR ES SALAAM, HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA

clip_image001Lori la mafuta likiwa limelidondokea gari dogo baada ya kutoke ajali katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es salaam ikihusishwa na daladala la abiria.

 Ajali mbaya inayohusisha Lori la Mafuta, Daladala pamoja na Gari aina ya Prado imetokea mapema leo maeneo ya Chang’ombe Machinjioni kwenye mataa Jijini Dar es Salaam baada ya dereva wa dalalala ambayo haikuwa na abiria kuingia vibaya katika makutano ya barabara na kusababisha dereva wa lori kugonga daladala na kuangukia Prado kama ionekanavyo pichani akijaribu kukwepa na kusababisha madhara.
Hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha katika tukio hilo isipokuwa majeraha ya kawaida yamewapata madereva husika, Wananchi wameonekana eneo la tukio wakichota mafuta ya mawese yaliyomwagika kutoka kwenye lori lililopata ajali na mpaka sasa hatua zote za tahadhari zimeshachukuliwa.

picha kwa hisani ya  http://differentsourcestz.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post