Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo Ikulu, Dar Es salaam.
Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari mwaka huu.
Rais Kikwete alipokutana mara ya mwisho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi Rais wa zamani wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana asigombee katika uchaguzi mkuu huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
Tags
HABARI ZA KITAIFA