Unknown Unknown Author
Title: POLISI MTWARA IMETOA ONYO KALI KWA WANANCHI KUHUSU VURUGU WALIZOPANGA KUFANYA KESHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kupitia safari redio mtwara,Kamanda wa polisi mkoani Mtwara  alisikika akitoa tahadhari kwa wananchi wenye hasira kali dhidi ya m...

Kupitia safari redio mtwara,Kamanda wa polisi mkoani Mtwara  alisikika akitoa tahadhari kwa wananchi wenye hasira kali dhidi ya mustakabali wa suala la gesi na nia ya serikali kwa maendeleo ya watu wa kusini...


Licha ya serikali kutumia gharama nyingi kuendesha kipindi cha BARAGUMU LA MSIMBATI kupitia kituo chake cha habari cha TBC ambacho katika kipindi hiki ni kama nyenzo ya kutoa elimu kwa wananchi wa tanzania hususani KUSINI , wananchi hao wameonekana kutoelewa na kutokubaliana moja kwa moja na serikali....

Wananchi manispaa ya Mtwara Mikindani wameaswa kununua mahitaji yao ya umuhim na kuweka ndani kwa siku ya leo kwani kwa siku ya kesho huduma za kijamii zitasimama ama zisipatikane moja kwa moja....
Kuna uwezekano mkubwa wa maduka mbali mbali ya vyakula,masoko,usafiri wa umma kama dala dala,boda boda na bajaji kusitisha  huduma kutokana na TAMKO la wanaharakati na wakereketwa wa gesi na mustakabali wa mtwara na kusini ya kwamba huduma hizo kesho zisimame na watu wawe macho kufuatilia mjadala wa hotuba ya waziri wa nishati na madini BUNGENI na iwapo hawataona la maana kwenye hotuba hiyo basi wataamua lao la kufanya...
Wanamshangaa RPC kukimbilia SAFARI RADIO kutoa tamko hilo kwani wao hawajapanga kufanya vurugu za aina yoyote zaidi ya kutaka haki itendeke
Wanasema kwa kuwa serikali ya CCM imeamua kutumia ubabe basi na wao wataonesha ya upande wao kwa MASLAHI YA VIZAZI VYAO VIJAVYO...

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top