Katika hali ya kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliliambia bunge jana jioni kwamba serikali imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.
Waziri Nchimbi alisema kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa....
Alisema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.
Huenda azimio hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Ikumbukwe ni hapo juzi tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kudhibiti wapinzani kuiimarisha CCM.
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.