Mwenyekiti wa TFF mkoa wa Lindi Ndg Ndulane akikagua Timu katika mechi hiyo. (Coast 1 – Kariakoo Fc 0, P( 6 – 7)
Timu ya Kariakoo fc leo ilishuka dimbani kumenyana na Timu ya Coast ya mjini Mtwara kumalizia mchezo wa pili, Mchezo wa awali Kariakoo Fc wa liibuka washindi kwa Ushindi mwembamba wa Goli 1 – 0 ndani ya Uwanja wa Ilulu Mjini Lindi.
Hadi Kipindi Cha Kwanza kinamalizika katika Mchezo huo uliokuwa na Uchezaji wa kuviziana uliisha kwa matokeo ya bila kufungana. Wakati huo uwanja wa umoja ulikuwa umefurika washabiki wapande zote mbili ilhali Kariakoo walikuwa wageni katika Uwanja huo lakini walijitokeza kwa wingi kuipa support timu yao.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Timu ya Coast Kiliandama lango la Kariakoo na Kufanikiwa Kupata Penalt baada ya Beki wa Kariakoo Fc kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari alipokuwa anajarippbu kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa languni mwake. Coast walifanikiwa kufunga penalt hiyo na kuongoza kwa goli 1 – 0.Hadi kipenga cha mwisho matokeo hayakubadilika na kuamuliwa kupigwa mikwaju ya Penalt ambayo Kariakoo Fc wali pata Penalt 7 na Coast walipata Penalt 6 hivyo Timu ya Kariakoo Fc kuibuka na Ushindi katika mchezo huo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.