Kulia ni Dkt Ferdinand Masau, enzi za uhai wake, akimuonesha mgeni toka Texas Childrens Hospital ya Marekani baadhi ya vifaa katika taasis yake ya Dr Ferdinand Masau Heart Institute aliyokuwa ameianzisha na kuanza kujenga huko Mbweni Mpiji nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Hii ilikuwa Oktoba mwaka jana
Mtaalamu wa magonjwa ya moyo Dkt. Ferdinand Masau, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Aga Khan, iliyopo Upanga jijini Dar es Salaama alikokuwa anatibiwa.
Habari hizo zimethibitishwa na marafiki wa karibu wa daktari huyo bingwa ambao hata hivyo hawakuwa tayari kutajwa majina kwa maelezo kuwa, wasemaji wa tukio hilo ni wanafamilia.
Maelezo kama hayo yalitolewa pia na mmoja wa maofisa wa hospitali ya Aga Khan, akisema wanafamilia ndio wanaoweza kuzungumzia taarifa za kifo cha mpendwa wao.
Enzi za uhai wake, baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaa nje ya nchi, alirejea nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuanzisha taasisi ya moyo, akilenga kuwasaidia Watanzania wengi ambao kwa muda mrefu walikuwa wakikosa tiba ya uhakika nchini, hivyo kukimbilia nje ya nchi, hasa India.
Hata hivyo, ndoto zake ziliyumba kwa kiasi fulani kutokana na kukosa majengo ya uhakika kwa ajili ya taasisi yake, hivyo kulazimika kupanga katika majengo ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambako baada ya kudaiwa kushindwa kulipa kodi, mali zake ikiwa ni pamoja na vifaa na samani zote zilizokuwa katika taasisi hiyo zilipigwa mnada. Baadaye aliripotiwa kuibuka upya na kuanza kuwekeza taasisi nyingine ya magonjwa hayo eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.