Unknown Unknown Author
Title: Dc Kilwa sahani moja na wazazi wasiopeleka watoto shule
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega Na Abdulaziz Video,Kilwa MKUU wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Abdalah ulega ameonya kuwa hatakuwa n...

E82A4289Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega

Na Abdulaziz Video,Kilwa
MKUU wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Abdalah ulega ameonya kuwa hatakuwa na msamaha kwa mzazi yeyote atakayeshindwa kumpeleka mtoto wake kuanza kidato cha kwanza kwa kisingizio cha umaskini wa kipato.

Akizungumza katika mahojiano na Fahari ya Kusini blog ya jamii, Mkuu huyo wa wilaya amesema kumekuwa na visingizio vingi kutoka miongoni mwa wazazi wanapo himizwa kuwapeleka watoto wao shule kwa madai kwamba hawana uwezo.
''Ukiwafuatilia watoto utasikia wazazi wanaanza utetezi Sina Uniform, Sina ada mara viatu na visababu vingi hii mwandishi siwezi kuliachia watoto hawa wataishi vipi baadae Wapo wakuu wa wilaya, madaktari, walimu wa baadae kwa nini tuwasitishie maisha yao. Hii siwezi kukubali na Nimeagiza na si kuagiza tu nitafuatilia
kuhakikisha watoto wanaelimika'
Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa endepo katika familia
kutakuwepo na mzazi hasiye jiweza, kinachotakiwa ni kuchukua hatua ya kumpeleka mtoto wake shuleni kwanza na kwamba mambo mengine yakiwemo ya ada na sare ya mwanafunzi yataendelea kutekelezwa taratibu wakati mwanafunzi akiendelea na masomo
'''Sasa kilwa Inapata mrahaba wa gesi ya songosongo takriban Milioni 100 na hivi karibu mambo yakienda vizuri Halmashauri itakuwa inaingiziwa Karibu milioni 300 kutokana na gesi kwa mwezi na Wakubwa. Madiwani wamepitisha kupitia baraza la madiwani kuwa mapato hayo aslimia 35 iende katika kuboresha elimu Je nikiacha raslimali za Kilwa zitachukuliwa na wageni wenyeji wakiwa watumwa...Kwa hili wazazi nitaenda nao sambamba na timu yangu ipo imara...Alimalizia Ulega
Sambamba na hayo nilipopata habari hiyo niliweza kubaini kuwa hadi
kufikia juma lilopita, jumla ya wanafunzi 414 wakiwemo wavulana 316
wasichana 98 waliochaguliwa kuingia kitado cha kwanza mwaka huu
walikuwa bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top