Mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa yanga walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 3 kupitia kwa Jeryson Tegete.
Coastal union walisawazisha goli lao kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Abdi Banda na mpira kutinga moja kwa moja katika nyavu za yanga na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Kwa matokeo hayo ya leo yanaitoa Coastal katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya tatu inayoshikiliwa na Kagera Sugar.
MICHEZO MINGINE.
Goli la kiungo wa zamani wa Azam fc, Mtibwa sugar na Simba sc Salum Machaku limeipa uhakika Azam fc wa kushika nafasi ya pili na kuwapa matumaini Simba sc yenye point 39 wakiwa na michezo mitatu kuchukuwa nafasi ya 3.
Machaku ameiwezesha timu yake ya Polisi Morogoro kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya Kagera sugar wanaoshika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 40 huku wakibakiwa na michezo miwili mkononi.
Matokeo ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro na kushuhudia Machaku akiandika goli katika dakika ya 63, imeifanya Polisi morogoro waendelea kungoja michezo ya Mgambo JKT ilikujua hatima yao ya kusalia ama kushuka daraja.
Wakati Polisi moro wakiongeza siku, wenzao African lyon wamekuwa wa mwanzo kushuka daraja baada ya kubali kufungwa goli 2-0 toka kwa Mtibwa sugar mchezo uliochezwa katika uwanja wa Manungu.
MATOKEO YA MICHEZO YA LEO.
YANGA 1-1 COASTAL UNION
POLISI MOROGORO 1-0 KAGERA SUGAR
JKT RUVU 1-2 PRISONS
MTIBWA SUGAR 2-0 AFRICAN LYON
RUVU SHOOTING 0-0 JKT OLJORO
POLISI MOROGORO 1-0 KAGERA SUGAR
JKT RUVU 1-2 PRISONS
MTIBWA SUGAR 2-0 AFRICAN LYON
RUVU SHOOTING 0-0 JKT OLJORO
Tags
SPORTS NEWS