WAKULIMA WAKOROSHO WALIA NA SOKO


Na. Mwanja Ibadi Lindi
JUMLA ya kilogramu milioni 17, 676 416 kati ya kilogram 33, 232468 za korosho za ghafi zilizo kusanya na vyama vya msingi kutoka kwa wakulima  mkoani Lindi kwa mfumo wa stakabadhi ghalani bado zimeludikana kwenye maghala ya vyama hivyo kutokana na kukosa wanunuzi.
Hayo yamebainishwa na kaimu afisa ushirika mkoa wa Lindi Saidi Munjai wakati alipokuwa anatoa taarifa ya mwenendo wa ununuzi wa  zao hilo msimu 2012/13 kwenye mkutano wa wakulima na wadau wa korosho uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi jana.
Amesema kuwa kati korosho hizo ambazo hazijanunuliwa zenye thamani ya jumla shs milioni 19,557,690,000 wilaya Nachingwea ndiyo inayoongoza  kwa kuwa na kilo 6,413,412  ikifuatiwa na Ruangwa wenye kilogramu 4,243,975 huku wilaya ya Liwale ikiwa na 3,782,467.
Amezitaja wilaya nyingine kuwa  Lindi vijiji wenye kilogramu 1,899,977 ikifuatiwa na wilaya Kilwa ambayo ina kilogramu 872,555 na  manispaa ya Lindi yenye kilgramu 478,990.
Taarifa hiyo ya kaimu afisa ushirika  iliibua maswali mengi  na kusababisha mabishano makali  kati ya wakulima, wadau wa korosho , ofisi ya ushirika mkoa  na chama kikuu cha ushirika Ilulu ambayo hata hiyo hakuna majibu yaliyotolewa ya kuwaridhisha  wajumbe hao na hatimaye kufikia uamuzi wa uhairisha kikao hicho   na kuteua tume ya watu 12 kwenda kuonana na rais kuhusiana na hatima ya soko la korosho za wakulima mkoani Lindi.




Previous Post Next Post