Na. Mwanja Ibadi Ruangwa
UKOSEFU wa gesi kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya wilaya Ruangwa mkoani Lindi ni moja ya changamoto zinazochangia kukwamisha zoezi la utoaji chanjo ya watoto ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha na kichomi( PCV na Rorotavirus) inayoendelea hapa nchini.
hayo yameelezwa na mratibu wa chanjo wilaya hiyo Joyse Mchopa wakati alipokuwa anazungumza na mwaandishi wa habari aliyetembelea wilayani humo jana.
mchopa alisema kuwa zoezi la chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kuhara na kichomi inayotolewa kwa watoto wenye umri wa wiki sita chanjo ya kwanza na wiki 10 chanjo ya pili na ya tatu wiki 14 imekwama kwa baadhi ya vituo kutokana na kukosekana kwa mitungi ya gasi kwa ajili ya majokofu ya kuhifadhia dawa.
alisema chanjo hiyo inawalenga watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja ambao hawajapata chanjo kabisa na kwamba watoto hao wataepuka kupata hatari ya magonjwa.
alisema lengo la chanjo hiyo ni kuwawezesha watoto kupata kinga ya mwili ambayo itasaidia kupambana na maradhi mbalimbali ambayo ni kikwazo kwa ukuaji na maisha yao kwa ujumla.
mchopa alisema chanjo hizo zna mkinga mtoto kuambukizwa na magonjwa zaidi ya tisa ambayo ni kifua kikuuu, kupooza, surua, donda koo, kichomi , homa ya manjano, kifaduro, kuharisha,pepopunda, polio na uti wa mgongo,
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Rebeun Mfune alikiri kuwepo kwa tatitzo la ukosefu wa gesi kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya.
mfune alisema kuwa halmashauri imeanza kulifanyia kazi suala hilo ili kuhakikisha kuwa watoto wanaostahili kupata huduma wanapata kwa wakati.