Leo ikiwa ni siku ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwa waumini wa dini ya Kiikristo, sikukuu hiyo imeingia dosari kwa wale wanaopenda kutembelea sehemumbali mbali za miji, Mvua kubwa iliyonyesha mjini hapa imefanya watoto na watu wazima kukaa majumbani mwao na kusherehekea sikukuu hiyo kwani haikuwa kazi rahisi kutoka na mvua hiyo iliyo dumu kwa masaa kadhaa na kutengeneza ma bwawa ya muda. kama ilivyo sehemu nyingi suala la miundombinu ni tatizo kwani maji yanashindwa kupita katika mifereji au sehemu zingine mifereji kuzidiwa na uwingi wa maji hayo.
Tags
HABARI ZA KITAIFA