Lindi veterani wali wakaribisha majirani wao wa Mkoa wa Mtwara katika bonanza liliofanyika Mjini Lindi Ndani ya Uwanja wa Ilulu siku ya Ijumaa na Lindi kuibuka kidedea kwa kuwachabanga magoli 2 – 1. Licha ya kuwa na kikosi nusu cha wachezaji ambao wengi wao wako safarini Arusha Katika Bonanza lingine litakalochezwa Leo Siku ya Pasaka, lakini Waliweza kuwamudu vilivyo na kuonesha kandanda safi kabisa dhidi ya wapinzani wao hao.
Hadi kipindi cha Kwanza kinaisha walikuwa sawa kwa goli 1 – 1. Kipindi cha pili kilianza kwa Lindi Veterani kupiga pasi za hapa na pale na kuweza kufunga goli la pili kwa kutumia winga ya kulia na mfungaji kujitwisha kichwa maridadi kabisa kilicho muacha mlinda mlango aikuduwaa asijue la kufanya na kufanya ubao wa matangazo kusoma 2 – 1 hadi mwisho wa mchezo.
Tags
SPORTS NEWS