Baraza kuu la Waislam Mkoa wa Lindi limetoa msaada wa Vifaa vya Ujenzi kwa ajili ya kuunga jitihada za waislamu wa Kata ya Nachingwea na Jamhuri, Manispaa ya Lindi baada ya kujitolea kuchangia ujenzi huo ili kuimarisha elimu ya Dini
Vifaa hivyo ikiwemo Bati, saruji, rangi na gharama za ufundi vyenye
thamani ya Tshs Milioni 2 laki tatu (2,300,000/=) vimekabidhiwa na
Katibu wa Bakwata mkoa, Alhaj Abdillah Salum kwa maalim wa Madrasa hiyo ya Al Rijala Musalam, Ustadh Abdulwahab Manzi
Akikabidhi Vifaa hivyo,Alhaj Abdillah aliwataka waislamu mkoani humo kujitoa na kuchangia ukuaji wa elimu ya Dini ya Kiislam kwa vijana na watoto ili wakue katika maadili yaliyo mema
'' Waislam tujitoe kushangia elimu hii kwa muskabali wa maisha yajayo
mambo mengi yanatokea kutokana na jamii nyingi kutofuata maadili na mafundisho ya dini ni lazima tuamke na tushikamane katika ibada
kuombea Nchi yetu Amani''alisema Alhaj Sambamba na msaada huo pia aliiomba serikali kurudisha na kutenga katika mipango yake ya elimu kwa kutoa fursa kwa elimu ya dini kufundishwa mashuleni kutokana na muda mchache anaopata mtoto katika kupata elimu ya Dini kwa siku za jumamosi na jumapili.
Akipokea msaada huo Ustadh Abdulwahab Manzi aliishukuru Baraza hilo baada ya kuona juhudi za waislam kuchangia ujenzi huo ambapo
alibainisha kuwa msaada huo utakamilisha kazi ya Ujenzi huo huku
akitoa wito kwa waislamu wengine Nchini ambao wamejaliwa kupata uwezo kuimarisha elimu ya Dini ikiwa pamoja na kujitolea kuchangia madrasa pamoja na Misikiti ili Waumini wapate fursa ya kusoma na kuabudu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA