JE ULIMISS SEHEMU YA 9 YA SIRI YA MTUNGI? HII HAPA

Kupotea kwa pikipiki yake nje ya nyumba ya ufukweni ya Lulu kunamfanya mpiga picha Cheche kuchanganyikiwa. Itakuwaje kama Cheusi atagundua uhusiano wake na Lulu? Cheche anarundika oungo juu ya uongo. Dafu anaahidi kumsaidia kuitafuta pikipiki -- lakini kwa sababu tu anahisi kwa kufanya hivyo atakuwa karibu zaidi na Lulu.
Wakati huohuo, tangu Nusura alipoolewa na Mzee Kizito, Duma amekuwa hana uelekeo na maisha yake. Kovu anamtambulisha kwa mfanya biashara aitwaye Golden kule kwenye kigrosari cha Tula. Lakini Kovu anapolewa na kumtukana bibi yule, Duma anamgeuka na kumtetea Tula -- kitu kinachomfanya yeye na Tula wagundue kuwa wana mambo yanayofanana.
Duma hana wasaa wa kukaa nyumbani, na muda si mrefu mdogo wake, Stephen, anachoshwa na masomo na kuelekea maskani kukutana na Max.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post