Zaidi ya Wakazi 600 wa Manispaa ya Lindi watanufaika na Ajira mara
utakapokamilika Ujenzi wa Kiwanda cha Simenti kilichoanza hatua za
awali za Ujenzi wake huku Tayari zaidi watu 250 wakiwa wamepata ajira katika hatua za awali baada ya kuanza kwa kazi hiyo hivi karibuni Akizungumza na Wakazi wa Manispaa ya Lindi mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa kiwanda hicho kilichoanza ujenzi kufuatia Upatikanaji wa Gesi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara,Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alitoa wito kwa Wazazi na walezi kuongeza jitihada za kusomesha watoto ili wanufaike na ajira zitakazopatikana kutokana Uwepo wa Viwanda na shughuli mbalimbali zinazotokana na Gesi ikiwemo Upanuzi wa Bandari ya Lindi ya Mji wa Lindi.
Maeneo ya Machole Manispaa ya Lindi ambapo alielezwa kazi
inavyoendelea na ajira zilizopo kwa sasa Sambamba na Gesi ya Mtwara, Waziri Membe alibainisha kuwa Kampuni ya Satoil ya Norway tayari imegundua uwepo wa Gesi nyingi umbali wa Km 85
baharini kutoka manispaa ya Lindi na kupatikana kwa gesi hiyo, Serikali tayari Imeshaingia mikataba ya Uchimbaji wake
‘’’’Gesi hiyo iliyogunduliwa na kampuni ya Satoil itasaidia maendeleo
ya Lindi kwa kuwa kutajengwa kiwanda cha Mbolea, Kiwanda cha vifaa vya plastiki aina zote pamoja na Upatikani wa uhakika wa nishati ya Umeme alimalizia Membe kwa kusema Lindi Kucheleeeee!!!!!”””
Industries,Bw Valerian Magembe alibainisha kuwa kazi ya Ujenzi wa
kiwanda hicho itakamilika na kuanza Uzalishaji June 2014 ambapo zaidi ya wananchi 600 watanufaika na Ajira na kueleza kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 500 kwa siku Ndg Waandishi mipango yetu iko vema kama mnavyoona kazi inavyoendelea na tayari Maji na Umeme ndio tunakamilisha, Wana Lindi wakae mkao wa kula kwa kupata ajira na ongezeko la pato la kila mdau kwa sekta yake…Na pia nawahakikishia kiwanda hiki ni cha kisasa na hakutokuwa na uharibifu wa Mazingira kutakuwa na mtambo wa kudhibiti Vumbi..Tumejipanga vilivyo…Alimalizia Bw Magembe.
Kazi za Ujenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni ya Wazawa ya Meis Industries kinatarajiwa kuzalisha tani 500 kwa siku
kitakapokamilika huku tayari ajira zaidi ya 250 zimetolewa kwa wakazi wa mji huo kwa awamu ya kwanza ya kazi za Ujenzi.
Tags
HABARI ZA KITAIFA