WAMA YASAIDIA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI VIFAA TIBA

Wama yakabidhi vifaa kwa Hospital ya mkoa wa Lindi
vifaa tiba (4)Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)Katika kusaidia sehemu kubwa ya Jamii na makundi yenye kuhitaji msaada hususan Wanawake,watoto na wasio na uwezo ufadhili wa Taasisi mbalimbali Nchi Za Nje ili Kuboresha Huduma za Afya hapa Nchini Imetoa msaada wa Vifaa tiba kwa Hospital ya Mkoa wa Lindi.vifaa tiba (6)Hayo yamebainika katika Hafla fupi ya kukabidhi Vifaa tiba kwa Vyenye thamani ya Milioni 700 vilivyotolewa na Shirika la Project Cure la Marekani baada ya Taasisi hiyo kuchangia na leo kukabidhiwa kwa Vifaa hivyo kwa Mkoa huo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae Pia ni Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete kueleza kuwa licha kukabidhi msaada huo misaada zaidi ya WAMA ipo katika nyanja za elimu, afya pamoja na maendeleo ya wanawake katika mikoa yote Nchini.
vifaa tiba (7)Aidha alibainisha kuwa pamoja na taasisi ya WAMA kupata mafanikio
katika kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto, mapambano dhidi ya Malaria na UKIMWI, chanjo kwa watoto ikiwemo ya ugonjwa wa Nimonia, mimba kwa wanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wa kike hapa nchini Pia ametoa wito kwa Wakazi wa Lindi kusimamia Elimu ya Watoto.
vifaa tiba (1)Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Project Cure la Marekani.Bw Abdu Kimario ameipongeza taasisi ya WAMA kwa mchango wake katika jamii hasa kuboresha elimu, huduma za afya pamoja na mapambano dhidi ya mimba za udogoni kwa wanafunzi wa kike na kuwaendeleza wajasiriamali wa kike nchini na kubainisha kuwa Vifaa kama hivyo vilivyokabidhiwa leo pia vitakabidhiwa katika mikoa mingine Nchini Hivi Karibunivifaa tiba (3)Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Dr Richard Boniface alieleza jinsi msaada huo utakavyosaidia kufuatia kutowepo kwa huduma ya X-ray kwa zaidi ya mwaka mmoja hata hivyo pamoja na msaada huo pia aliomba ufadhili zaidi wa Elimu kwa watumiaji wa Vifaa tiba hivyo Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na Mashine ya X-ray pamoja na vifaa vyake vyote,Mitambo ya kitanda maalum cha ICU Kwa ajili ya wagonjwa mahututi,Mitungi ya gesi ya Oxygen ambayo itasaidia kutoa huduma ya dharura hasa wakati Umeme umekatika, Vifaa na mitambo kwa ajili ya huduma za kinywa na meno, Vifaa vya upasuaji mdogo na mkubwa,Ultra sound machine, Taa,meza na mashine ya Usingizivifaa tiba (9)Wazee wausalama Barabarani wakishauliana Jambo.
Previous Post Next Post