Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52, hajapata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo tangu alipoteuliwa kuchukua mahala pa Roberto Di Matteo mwezi Novemba mwaka uliopita.
Katika mechi nyingi zilizopita za Chelsea, mashabiki wa klabu hiyo hawakuficha hisia zao za kutaka kocha huyo kufutwa kazi.
Rafael Benitez, amesema kuwa atakihama klabu ya Chelsea mwezi Mei mwaka huu na kutaja uamuzi wa kuumpa wadhifa wa kaimu kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.
Katika mahojiano na BBC, Benitez amesema uamuzi wa Chelsea wa kuumpa cheo cha kaimu kocha wa klabu hiyo ilikuwa kosa kwa sababu yeye ndiye kocha mkuu kwa sasa.
Amesema mashabiki wao hawajawapa msaada wanaohitaji na hivyo ameamua kuondoka mwisho wa msimu huu.
'' Mashabiki sasa hawana sababu ya kunung'unika kunihusu'' Alisema kocha huyo.
Tags
SPORTS NEWS