Imeelezwa kuwa Baadhi ya mila na desturi zilizopitwa na wakati
ambazo zinaendelezwa hivi sasa zinachangia kwa kiasi kikubwa tabia ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ya ushirikishwaji watoto wa kike kwenye vikao vya kifamilia vinavyojadili ndoa na Talaka ikiwa pamoja na kuchangia maamuzi Pamoja na kila jamii kuzingatia ,kulinda na kudumisha mila na desturi zake lakini kuna haja ya kuzichambua upya ili kuzipata zile nzuri zinazofaa kwa na kuhakikisha zile zinazokandamiza wanawake zinatokomezwa.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Masoko wilayani Kilwa, Bw Peter Amos Malekela alipokuwa akifunga na kufungua katika Midahalo miwili iliyofanywa katika Jimbo la Kilwa kusini na Kilwa kaskazini iliyoendeshwa na Mtandao Mwavuli wa Asasi zisizo za Kiserikali Wilayani Kilwa (Kingonet) Malekela aliwataka wanawake kuachana na mila hizo kandamizi na badala yake wajitokeze kufanya kazi za maendeleo ikiwemo kugombea nafasi mbalimbali masuala ya siasa ili wawe miongoni
mwa viongozi wa kufanya maamuzi mbalimbali katika maeneo yao.
“Mafanikio yoyote mwanamke ndiye anastaili kupongezwa kutokana na jukumu alilonalo katika familia, hivyo ni vyema taasisi za mbalimbali
na wadau wa maendeleo na wana siasa wakawaonyesha wanawake njia za kuleta mbadiliko katika familia na taifa kwa ujumla’.Alimalizia
Malekela
Awali akitoa maelezo mafupi ya Mdahalo huo,Katibu Mtendaji wa
Kingonet,Omary Mkuwili alieleza kuwa Asasi yake ipo kwa ajili ya kutoa elimu mbalimbali kupitia midahalo kwa Lengo la kufikisha elimu na kupokea Mawazo mbalimbali kwa wasiopewa nafasi kusikika ili kuchangia maendeleo ya Kilwa na Mkoa wa Lindi.
Aidha aliwaasa Washiriki wa Mdahalo huo kuachana na Imani zilizo
potofu za kujenga akilini kuwa Mwanamke akifanikiwa katika maisha
wanadhani yupo mwanaume nyuma yake amemwezesha mafanikio hayo lakini hapana wapo wanawake mwenye uwezo wa kiakili, mali na utendaji kuliko wanaume huku akibainisha kwa kiasi kikubwa ndio viongozi na washauri wakuu kujenga utamaduni na kusisitiza kusaidia na kuchangia shughuli za kuwajengea uwezo wanawake ili kuharakisha maendeleo.
Midahalo Hiyo miwili iliyofanyika katika Kata ya Chumo na Kilwa Masoko ikiwa na lengo la kujadili suala la jinsia inavyochangia maendeleo na kuendeshwa na mtandao wa mashirika yasiyo kuwa yakiserikali wilaya Kilwa(KINGONET) kwa ufadhili wa The foundation for the civil Society
Tags
HABARI ZA KITAIFA