Unknown Unknown Author
Title: YANGA YAWATANDIKA TENA LEOPARD
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Yanga SC imeilaza mabao 2-1 Black Leopard ya Afrika katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Mabao y...

Yanga SC imeilaza mabao 2-1 Black Leopard ya Afrika katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Said Bahanuzi ‘Spider Man’ dakika ya tatu na Jerry Tegete dakika ya 54 kwa penalti. Huo ni ushindi wa pili kwa Yanga dhidi ya timu hiyo, baada ya awali kuwalaza 3-2 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga inarejea Dar es Salaam kesho, tayari kwa mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mzunguko wa pili dhidi ya Prisons ya Mbeya, Jumapili Uwanja wa Taifa. Leopard pia wanarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba kesho, Uwanja wa Taifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top