Unknown Unknown Author
Title: WASHIKIRIWA NA POMBE HARAMU LITA 300 HUKO WILAYANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz,Lindi WATU wanne wakiwemo watumishi wa basi ndogo aina ya Hiace,wakazi wa mkoa wa Mtwara,wanashikiliwa na Polisi mkoani Lin...
gongo 1
Na Abdulaziz,Lindi
WATU wanne wakiwemo watumishi wa basi ndogo aina ya Hiace,wakazi wa mkoa wa Mtwara,wanashikiliwa na Polisi mkoani Lindi,kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kuwatelekeza abiria njiani kwa ajili ya kwenda kupakia na kubeba pombe haramu ya moshi (gongo). Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani hapa, George Mwakajinga,zinaeleza watuhumiwa hao wote wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mwakajinga amewataja wanaowashikilia kuwa ni pamoja na dereva na kondakta wa Hiace, Shaibu Daudi (30),John Mbena Saidi (25),Mariamu
Yassini Mautila (36) wakazi wa Ligula,na Habiba Maulidi Sijaona (28) Wafanyabiashara ya Pombe ya moshi (Gongo) mkazi wa mtaa wa
majengo,Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na kitendo
kilichofanywa na wafanyakazi wa gari hiyo kuwashusha na kuwatelekeza njiani abiria waliokuwa wamewabeba kuelekea mkoani Mtwara,na kwenda kijiji cha Ruhokwe kilichopo wilaya ya Lindi,kubeba pombe haramu ya moshi (gongo).
Mwakajinga akasema Hiace hiyo,ambayo mlango mkubwa wa nyuma umeandikwa neno lisemalo,Simba wa Yuda,yenye namba za usajili T 436
BJV, inamilikiwa na mfanyabiashara aitwae D.D. Chigumila wa mjini Mtwara,ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 20,wakitoka mjini Lindi kwenda mkoani Mtwara.
“Siku hiyo hii ilikuwa ikirejea mkoani Mtwara, ambapo iliwabeba abiria
na walipofika eneo la kijiji cha Mnolela, Lindi vijijini,dereva na kondakta wake huyo,waliwatelemsha njiani abiria waliokuwa wamewabeba bila ya kuwapa msaada mwingine na kuondoka zao”Alisema Mwakajinga.

Kamanda huyo wa Polisi mkoa akasema kutokana na kitendo walichofanyiwa
abiria hao, walichukuwa uwamuzi wa kupiga simu kwa askari wa kata ya
Mingoyo, wilaya ya Lindi,ambapo waliwafuatilia na kufanikiwa kuikuta gari hiyo kijiji cha Ruhokwe,ikiwa imebeba madumu (15) ya pombe ya gongo yenye ujazo wa Lita 300.
Wakizungumza na mtandao huu, baadhi ya abiria hao,akiwemo mke wa mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Lindi (LPC),Mrs Abdull -aziz,Devota Ng’itu,Lucy Aizaki,Madadi na Fatuma Mkaumba, wameiomba Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumnyang’anya leseni ya kuendesha gari kwa dereva huyo.
“Tulikuwa tukitoka mjini Lindi kwenda mkoani Mtwara, na tulipofika eneo la kijiji cha Mnolela dereva alisimamisha gari na kutueleza gari ni mbovu hivyo tutelemke watatuombea msaada gari nyingine, jambo ambalo halikuwa la kweli” Alisema Fatu Mkaumba. Abiria hao walisema mara baada ya kutelemka chini ili kutekeleza ombi la wafanyakazi, waliondoa gari na kuondoka zao,huku bila ya hata kuwarejeshea fedha walizozichukuwa za nauli walizolipa.
”Kwa kusema kweli ndugu yetu mwandishi wa habari,wafanyakazi hao wa
Hiace wametufanyia kitendo cha kinyama ambacho hakiwezi kuvumiliwa, ikizingatiwa muda waliotutelemsha njiani ni wa jioni ya saa 12:45” Alisema Mrs Abdull-azizi Mwakilishi wa Sumatra mkoani Lindi, Duncan Somi,ameuambia mtandao huu kwamba kwa kitendo kilichofanywa na wafanyakazi hao wa Hiace, kukatisha au kuwatelemsha na kuwatelekeza abiria njiani ni kosa chini ya kifungu cha (17) kifungu kidogo cha (1) {C} ambapo faini yake sio chini ya Sh,250,000/-

About Author

Advertisement

 
Top