Na. Christopher Lilai,Nachingwea
WAKATI Serikali ikipiga marufuku wanafunzi kufukuzwa shule na watoto wanaotarajia kujiunga na darasa la kwanza kukataliwa kwa kushindwa kulipa michango mbali mbali
Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wanaosoma shule ya msingi ya Mazoezi Nambambo,wilaya ya Nachingwea,mkoa wa Lindi wamelalamika kitendo cha uongozi wa shule hiyo kuwafukuza wanafunzi ambao hawajalipa michango mbalimbali inayohitajika shuleni hapo na kusababisha hadi sasa idadi ya watoto waliojinga darasa la kwanza kuwa chache.
Wakizungumza na mwananchi kwa nyakati tofauti Boniface Mnali mkazi wa Kilimanihewa alisema kuwa watoto wake wawili mmoja akiwa ni wa darasa la kwanza walitimuliwa shuleni hapo baada ya kutowasilisha michango ikiwemo wa mahindi kilo kuma na fedha taslimu kiasi cha shilingi alfu kumi na mia moja.
Mzazi huyo alisema kuwa baada ya kuona hali yake ya kifedha si mzuri alimwomba mwalimu mkuu wa shule hiyo ili atangulize nusu ya michango hiyo na kiasi kinahosalia kukamilisha muda mfupi ujayo lakini ombi hilo lilikataliwa.
“Kwa sasa kutokana na kuyumba kwa zao la korosho nilimwomba mwalimu mkuu akubali kuchukua nusu ya michango ili huyu mwananfunzi aendelee kupata masomo na baada ya kulipwa malipo ya korosho nimalizie lakini huyu mwalimu alikataa katakata na kuamua kuwatimua hawa watoto wote hata huyo anayetarajia kuanza darasa la kwanza”alisema Mnali.
Mzazi mwingine ambaye mtoto wake alikumbwa na timuatimua hiyo ni Regina Ashiru mkazi wa mtaa wa Uhindini ambaye mtoto wake anayesoma darasa la saba alitimuliwa salisema kuwa kama mzazi anasikitishwa na kitendo cha uongozi wa shule hiyo ya kuwatimua wanafunzi kwa kosa la wazazi kwani kuwafukuza watoto ni kuwanyima haki yao ya kujipatia masomo na kuwa jukumu la kugharamia masomo ni ya wazazi.
Akizungumzia malalamiko hayo Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Devota Mlonganile alikiri kuwatimua watoto hao kwa madai ya kusukuma upatikanaji wa michango kwani alikuwa anatekeleza maagizo ya kamati ya shule na kuwa swala la michango hiyo lilifahamika na kila mzazi na mlezi kuwa mara itakapofunguliwa shule kila mwananfunzi aje akiwa amekalisha michango hiyo.
“Haya yalikuwa ni makubaliano ya wazazi wote na kamati ya shule kwani michango hasa ya mahindi kwa ajili ya watoto wao na kuwa mwaka jana tulitumia njia ya kuwaandikia barua wazazi na walezi lakini hawakuleta michango lakini mwaka huu baada ya kuwatimua watoto tumeweza kukusanya kiasi cha kutosha”alisema Mlonganile
Makamu mkuu wa chuo cha ualimu Nachingwea ambacho ni wamiliki wa chuo hicho,Loius Letta aliulizwakuhusu malalamikao hayo alidai kuwa hana taarifa yeyote kuhusiana na malalamiko hayo licha ya kukiri kuwa alipata tetesi ya kuwa mwanawe angetimuliwa.
“Taarifa hii sijaisikia ila nakumbuka siku moja niliambiwa kuwa mtoto wangu alitaka kutimuliwa lakini kuna walimu walimwambia huyo mwalimu mkuu kuwa huyo motto haumjui kuwa ni wa makamu hivyo hakamwaacha”alisema Letta.
Naye Afisa elimu msingi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Makwasa Bulenga akizungumza kwa njia ya simu juu ya malalamiko hayo alisema hana taaraifa yeyote na kuwa kama shule hiyo inafanya hivyo ni kosa na kuwa atafuatilia kwa mwalimu wa shule hiyo.
“Kwa sasa nipo nje ya ofisi na taarifa hiyo sina lakini nitafika shuleno hapo nifuatilie nakushuru kwa taariafa yako kwani umenisaidia sana ”alisema Bulenga.
WANAFUNZI WAFUKUZWA SHULE KWA KUKOSA MICHANGO
Title: WANAFUNZI WAFUKUZWA SHULE KWA KUKOSA MICHANGO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Christopher Lilai,Nachingwea WAKATI Serikali ikipiga marufuku wanafunzi kufukuzwa shule na watoto wanaotarajia kujiunga na darasa la k...