Na Said Hauni na Aisi Sobo, Lindi.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Lindi,imekusanya maduhuri ya Sh,227,528,862.52 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato,na kushindwa kuvuka lengo lililojiwekea la Sh,348,386,500/-kwa kipindi cha miezi sita ya mwaka uliopita.
Takwimu hizo zimetolewa (leo) jana na mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Frank Magari,wakati akifungua kikao cha Baraza la madiwani, kilichofanyika ukumbi wa DDC mjini hapa.
Kabla ya kuanza kwa kikao hicho,Magari aliwaomba wajumbe kusimama ili kuwakumbuka wenzao waliotangulia mbele ya Haki (kufariki dunia) akiwemo Diwani wa kata ya Mwenge kwa tiketi ya CUF, Bilali S.Bilali,Mchumi wa Manispaa hiyo,Iddi Kalua na mwangalizi wa Ofisi (OS) Mwinyihalawi.
Mstahiki Meya huyo akifungua kikao hicho cha Baraza la Madiwani hao,akasema makusanyo hayo ni ya kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Decemba 2012.
Akasema katika kipindi hicho cha miezi sita,Halmashauri ya manispaa ya Lindi, ilipanga kukusanya maduhuri ya Sh,348,386,500/-lakini imeambulia kukusanya Sh,227,528,862.52 sawa na asilimia 65%.
Magari ametaja sababu zilizochangia kutofikiwa kwa lengo ni pamoja na kutolipwa kwa ada za leseni za Biashara kutokana na kuchelewa kuwafikishia mwongozo kutoka Serikali kuu,kutofikia muda wa malipo kwa minara ya simu kama mikataba yao inavyoelekeza pamoja na kutonunuliwa kwa zao la korosho za wakulima.
“Chanzo cha uhakika cha mapato ya halmashauri yetu ni vyanzo vya ndani,hivyo napenda kutoa wito kwa madiwani wenzangu na watendaji wote,kuhakikisha chanzo hiki kinatunzwa na kutafuta vipya vya ndani”Alisema Magari.
Akasema kwa kutumia makusanyo hayo ya ndani na fedha matumizi mengineyo,ikiwemo (OC) inayopatiwa Manispaa hiyo inaendelea na kazi ya kuimarisha usafi wa mazingira,ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifereji,kuzoa taka na kufyeka nyasi.
Pia amewasisitiza wakazi wa manispaa hiyo kwa ujumla wanasimamia na kushiriki Shughuli za usafi wa mazingira,yakiwemo yale yanayozunguka nyumba zao,ili kuepuka kero zitokanazo na uchafu pamoja na kuzuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kuzuilika.
“Hivi sasa Halmashauri yetu imeanza utaratibu wa kuzoa taka kwenye vizimba na zile za majumbani kwa kutumia vikundi,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Hivyo kila kaya iwe na utaratibu wa kuweka chombo cha kutunzia taka na kulipia gharama za uzoaji kwa viwango vilivyopangwa katika mtaa”Alisema Magari.
Aidha,mstahiki meya huyo amezidi kutoa wito kwa baadhi ya wakazi walio na mifugo kufuata Sheria zilizowekwa na serikali za mitaa na mamlaka ya miji ya mwaka 2008,ikiwa ni pamoja na kuwa na vibari kutoka mamlaka husika ambayo ni Idara ya mifugo.
MANISPAA YA YASHINDWA KUVUKA LENGO LA MAKUSANYO.
Title: MANISPAA YA YASHINDWA KUVUKA LENGO LA MAKUSANYO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Said Hauni na Aisi Sobo, Lindi. HALMASHAURI ya Manispaa ya Lindi,imekusanya maduhuri ya Sh,227,528,862.52 kutoka kwenye vyanzo vyake mba...