Na Hamisi Nasiri,Masasi
MADIWANI wa halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara wameshauriwa kupima afya zao kwa hiyari ikiwa ni pamoja na kuanza kuhamasisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya kondomu hatua ambayo itasaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayani humo.
Ushauri huo ulitolewa jana na mwenyekiti wa bodi ya korosho, Anna Abdallah wakati alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye kikao cha kawaida cha madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo mjini hapa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa suala la kupima afya ni la msingi kwa kuwa ni njia moja wapo ya kujitambua kiafya na pia inasaidia kutoa takwimu sahihi za watu waliombukizwa virusi vya ukimwi,na kudai kuwa iwapo jamii ikihamasishwa vema juu ya matumizi ya sahihi ya kondomu itakuwa na uwelewa wa kutosha wa namna ya kuweza kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi jambo litakalosaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Alisema kuwa Jamii bado haina uwelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya mipira ya kondomu hali inayochangia kuwepo kwa kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayani Masasi.
Alisema iwapo madiwani hao watakuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi juu ya suala la matumizi sahihi ya kondomu kwenye maeneo yao wanakotoka jamii inaweza kubadili tabia na kuanza kujitambua juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi hatua mabayo itasaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya ukimwi.
Mwenyekiti huyo alisema ipo njia mzuri ya kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa wa ukimwi ambayo ingesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi, aliitaja nji hiyo kuwa ni kuweka mabango katika maeneo mbalimbali ya mji huo yanayotoa maelezo juu ya athari za ugonjwa huo na njia mbalimbali za namna ya kuweza kujinga na maambukizi mapya ya virusi vya ukumwi jambo litakasaidia kuongeza uwelewa mpana kwa jamii dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.
“Hivi sasa tunatakiwa kuwa wawazi juu ya suala la ugonjwa wa ukimwi kwa jamii……hivyo ni razima kuhamasisha kwa nguvu zote ili jamii iweze kubadili tabia na hatimaye kuwa na uwelewa wa ukotosha wa namna ya kuweza kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi ili mwisho wa siku tuweze kupunguza idadi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi,” alisema Bi Abdallah
Wilaya ya Masasi inaongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi katika mkoa wa Mtwara,kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayni humo kwa sasa kutokana na takwimu ni asilimia 6.1 hivyo jitihada mbalimbali kutoka kwa viongozi wilayani humo bado zinahitajika katika kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.
Nae diwani wa kata ya mwenge Hamisi Mnela alisema endapo madiwani hao watachukuwa hatua ya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi itakuwa njia moja wapo ya kuhamasisha jamii kujitokeza katika kupima virusi vya ukimwi na kwamba hatua hiyo iyasaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo wilayani humo.
“Sisi tukianza kujitokeza kupima afya zetu hata jamii pia itahamasika kupima lakini kama sisi viongozi hatujitokezi kupima basi hata jamii haiwezi kuona umuhimu wowote wa kupima afya jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za mpambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi wilayani humo na kufanya maambikzi yaendelee kwa kasi,”alisema Mnela
KIKAO CHA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI MASASI
Title: KIKAO CHA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI MASASI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Hamisi Nasiri,Masasi MADIWANI wa halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara wameshauriwa kupima afya zao kwa hiyari ikiwa ni pamoja na kua...