Unknown Unknown Author
Title: WAANDAMANAJI WALA KICHAPO HEVI KUTOKA KWA POLISI, WANAFUNZI WA IFM...
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA KIKIJIWEKA TAYARI KUWAKABIRI WANACHUO WA IFM WANACHUO CHA IFM WAKIWA CHINI YA ULINZI TAYARI KWA KUPELEKWA KITUO ...
KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA KIKIJIWEKA TAYARI KUWAKABIRI WANACHUO WA IFMWANACHUO CHA IFM WAKIWA CHINI YA ULINZI TAYARI KWA KUPELEKWA KITUO CHA POLISIWanafunzi hao wakielekea kwenye kituo cha polisi huku wakiamriwa kunyoosha mikono juu baada ya kuwekewa mtego na kunaswa pamoja na kupigwa mabomu  kutokana na kulazimisha kufanyika kwa mkutano wao na kamanda Kova mbele ya kituo hicho cha Polisi
Wapo walioonja joto ya jiwe.. hebu angalia huyu kijana na yule askari aliyeinua kurungu juu Jiulize je kilifika mwilini au la kisha utapata jibu.



Na Mwandishi wetu:
BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa, Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.


About Author

Advertisement

 
Top