Unknown Unknown Author
Title: TAMKO LA CCM: HATUTAKI GESI IENDE DAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SUALA la wananchi kupinga gesi asilia inayovunwa kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara kupelekwa Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya C...
tz}ccm[1]
SUALA la wananchi kupinga gesi asilia inayovunwa kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara kupelekwa Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya Cham Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mtwara Mikindani kuungana na wananchi kupinga mradi huo, huku mbunge wake Hasnain Murji akisema yupo tayari kuvuliwa ubunge kwa kutetea maslahi ya wana-Mtwara.
Mwenyekiti wa CCM wa Manispaa hiyo, Ali Chinkawene amesema kuwa msimamo wa chama chake ni kuungana na wananchi kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam na kwamba Serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara badala ya Dar es Salaam.
“Tulipoona hali inakuwa tete, niliitisha kikao cha kamati ya siasa kujadili nini msimamo wa chama katika hili, kamati ya siasa wakasema hawawezi kukisemea chama kwa sababu chama ni wanachama hivyo nikaitisha kikao cha halmsahauri kuu ambapo pia tuliwaalika mabalozi wa mitaa” alisema Chinkawene
Alifafanua kuwa “Katika kikao hicho wajumbe walipinga kwa nguvu zote suala la gesi kupelekwa Dare s Salaam, wakaniambia niseme msimamo wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale maslai ya Wana Mtwara yatakapowekwa wazi na serikali”
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa msimamo huo sio wake binafsi bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho vinavyowakilisha wanachama na kwamba historia ya mikoa ya kusini jinsi ilivyonyimwa maendeleo ilitumika na wajumbe kujenga hoja yao hiyo.

“Wakati sisi hatuna umeme hakuna aliyefirikia kutuunganisha kwenye gridi ya Taifa…barabara ya kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam miaka 51 ya uhuru sasa haijakamilika, lakini bomba wanataka kujenga kwa miezi 18, hivi kuna Watanzania muhimu zaidi ya wengine?” alihoji Chinkawene akinukuu kauli za wajumbe wa kikao hicho
Alibainisha kuwa “Walizungumza mambo mengi, suala la kung’olewa kwa reli, kukatazwa kulima Pamba, kuuawa kwa kilimo cha Karanga, Mkonge, haya yote wanadai yamesababisha mkoa uendelee kuwa masikini na kwamba tumaini lao limebaki kwenye gesi, wamesema wapo pamoja na wananchi”
Katika hatua nyingine Murji jana alikutana na umoja wa vyama vya siasa vilivyoratibu maandamano na kuwapongeza rasmi kwa kazi nzuri walioifanya ya kuieleza serikali kuwa wana haki ya kutetea rasilimali yao na kuongeza kuwa yupo pamoja na viongozi hao.
Tofauti na ilivyokuwa awali sasa vyama hivyo vimefikia kumi baada ya kuongezeka kwa Chama cha Wananchi (CUF) na CCM, huku vyama vya awali vikiwa ni Chadema, NCCR-Mageuzi, SAU, TLP, APPT Maendeleo, ADC, VDP na DP, vikiwa na kaulimbiu ya gesi kwanza vyama baadeye, hapa hakitoki kitu.
Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kanisa la Pentekoste mjini Mtwara uliendeleshwa na mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa, Hussen Mussa Amri na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo akiwemo Chinkawene na mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa kutoka Mtwara mjini, (Nec), Godbless Kweka.
Murji alisema kwa kuwa yeye si mbunge anayewakilisha mawazo yake bungeni bali mawazo ya wananchi anaona bora aungane na wananchi ili kutetea maslahi yao.
“Nawapongeza viongozi wa vyama vya siasa kwa ujasiri na uthubutu wenu wa kutetea rasilimali hii (gesi)… tusidharau hata kidogo malalamiko ya wananchi…usilazimishe mawazo yako kuwa mawazo ya wananchi, hilo haliwezekani…nakubaliana na ninyi kuwa wachawi wa maendeleo ya kusini ni viongozi, tuache woga tushikamane” alisema Murji huku akishangiliwa na wajumbe
Alibainisha kuwa “Nipo pamoja nanyi na hata ikibidi nivue ubunge nipo tayari kufanya hivyo kwa maslahi ya wananchi….ni heri niondoke madarakani kwa heshima kuliko kuwa kiongozi kwa ufedhuli….tuache unafiki…wapo wabunge wenzangu wanasema wananchi wamekubali hivi ni kweli?”
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Uledi Abdallah ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtwara mjini alimpongeza mbunge huyo kwa kuungana na wananchi hao na kuahidi kumpa ushirikiano huku akisisitiza kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kutanguliza maslahi ya wengi.
“Tumefarikijika kuona wenzetu wa CCM na wewe mbunge wetu umeungana na sisi….tofauti zetu za kisiasa tuziweke kando, tusimamie rasilimali yetu” alisema Uledi.
mwisho















About Author

Advertisement

 
Top