Unknown Unknown Author
Title: SHAURI, NJECHELE KUWANIA UBINGWA WA MABARA KESHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF  INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa...
Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF  INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa iringa katika pambano la kirafiki la raundi nane katika ukumbi wa  D.I.D Hall uliopo mabibo mwasho.
Mratibu  wa pambano hilo Charles Christopher mzazi  ameeleza kuwa maaandalizi ya pambano yapo kamili na mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani  na wamepima wapo sawa kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza  pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo sawa kwa kupambana.
Mabondia watakaocheza utangulizi ni kama ifuatavyo HAMIS MOHAMED na  HARUNA MNYALUKOLO, PENDEZA SHOMARI atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO na KARIMU RESPECT, DOTO MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku ISSA OMAR akizipiga na  JUMA J KASHNDE.

Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe  ama bigright amethibisha kuwa kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa  na mabondia wapo katika hali nzuri ya kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi wa DID HALL mabibo mwisho kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL RAMADHANI SHAURI  na  SAID  NJECHELE


About Author

Advertisement

 
Top