Unknown Unknown Author
Title: PINDA KUZUNGUMZA NA WENYEKIVITI WA MITAA MTWARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, leo saa Sita mchana atafanya kikao katika Ukumbi wa Veta na wenyeviti wa mitaa wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani k...
Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, leo saa Sita mchana atafanya kikao katika Ukumbi wa Veta na wenyeviti wa mitaa wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kujadili kuhusu gesi.
Ni baada ya kumaliza kikao chake hapo jana na Wanaharakati, wanasiasa na viongozi wa dini.
Habari ambazo hazina shaka zinasema kuwa Pinda pamoja na mambo mengine atatoa msimamo mpya wa serikali kuhusu suala la mzozo wa gesi unaofukuta hivi sasa.
Inadaiwa kuwa jana Waziri Mkuu Pinda aliwasili mjini Mtwara na kukutana na makundi hayo ambapo inadaiwa katika kikao hicho kilichofanyika veta Mtwara, Pinda alisema serikali yake imekubali kilio cha wana Mtwara cha kutaka gesi kutosafirishwa.
Habari zainadai kuwa Pinda alisema Mitambo ya kufua umeme na kuchakata gesi itajengwa Mtwara badala ya kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Pia wazee hao waliiomba serikali kuwaachia huru watu waote waliokamatwa kufuatia vurugu zilizojitokeza juzi kati mjini Mtwara na juzi wilayani Masasi ili kurejesha amani katika maeneo hayo.
Habari kutoka Lindi na Mwandishi wetu Abdullaziz Ahmad zinadokeza kuwa serikali imeongeza polisi na magari ya maji ya kuwasha kusaidia kutuliza vurugu Mjini Masasi.
Mwandishi wetu ameshuhudia askari na magarihayo yakipita mjini Lindi na Kuelekea Masasi.
Tunaendelea kutafuta ukweli wa yaliyojadiliwakatika kikao cha wazee cha jana…. endelea kufuatilia kujua hatima yake.
source: KUSINI BLOG








About Author

Advertisement

 
Top