IDADI ya watu waliouawa katika vurugu za wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara imeongezeka na kufikia Tisa kutoka saba walioripotiwa awali. Mmoja aliyekuwa majeruhi na kulazwa hospitali ya misheni ya Ndanda ameripotiwa kupoteza maisha yake.
Ndugu wa karibu wa marehemu ameithibitishia mtandao huu kuwa ndugu yao huyo amefariki leo saa 9 usiku akiwa napatiwa matibabu hospitalini. Mchana wa leo mwendesha Bodaboda mmoja ameuawa kwa kupigwa na vitu vinavyosadikika kuwa ni risasi za moto na kupoteza maisha papo hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa polisi wakiwa katika gari walimminia risasi kijana huyo aliyekuwa anaendesha pikipiki yake. Taarifa kutoka hospitali ya Ndanda zinasema kuwa hadi sasa majeruhi wapo 12, nakwamba miili yao imetobokatoboka ishara walipigwa na risasi nawanendelea namatibabu.
Tayari waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi amewasili mkoani Mtwara akiambatana na Mkuu wa Polisi IGP Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (JWTZ) Davis Mwamunyange.
Habari zinasema kuwa viongozi hao watafanya kikao na viongozi wa Mtwara na badae kwenda Masasi kushuhudia hali ilivyo. Hata hivyo kuna habari kuwa Waziri Mkuu atawasili kesho mjini Mtwara kufuatia vurugu zinazoendelea ambazo zinachagizwa na kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.
Hayo ni mauaji ya kwanza kutokea kwa polisi kuua watu wengi kwa risasi za moto, hali inayoitia doa serikali.
source: KUSINI BLOG
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.