PICHA ZA VURUGU MTWARA MASASI
Na. Ahmeid Abdulazizi, Masasi
Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi kilichoko manispaa ya Mtwara/Mikindani yakoswa koswa kuchomwa moto hii leo kwa kile
kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia pamoja na kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara.
Vurugu hizo zilizoanza jana leo zimehamia wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo Inasemekana Askari mmoja wa Upelelezi wa jeshi la Polisi Ameuawa baada ya kujiingiza katika kundi na kubainika akiwapiga picha ambapo pia alikutwa na bastola 2 huku Nyumba ya Mbunge wa Masasi (Mama Kasembe), Vifaa vya Mahakama ya mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri nayo yateketezwa kwa Moto mchana hii leo katika vurugu za waandamanaji zilizoanza kwa waendesha Bodaboda kuanza kuandamana POLISI wakizidiwa
na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto ,
Taarifa za ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa
kufuatia simu za mkonononi za viongozi wa polisi kutopokelewa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Kassembe,Mbunge wa Masasi
Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa
kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es
Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.