Unknown Unknown Author
Title: NAIBU WAZIRI AKATAA SABABU ZA WATENDAJI WA (M) LINDI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Said Hauni na Aisi Sobo,Lindi. SERIKALI imekataa baadhi ya madai yaliyotolewa na watendaji wa Idara ya elimu, mkoani Lindi,kwamba matok...
002
Na Said Hauni na Aisi Sobo,Lindi.
SERIKALI imekataa baadhi ya madai yaliyotolewa na watendaji wa Idara ya elimu, mkoani Lindi,kwamba matokeo mabaya kwa mitihani kuhitimu elimu ya msingi na Sekondari,kumetokana na sababu mbalimbali zikiwemo migomo na idadi ndogo ya walimu.
Madai hayo yamekataliwa jana na Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia elimu,Kassimu majaliwa,alipokuwa akizungumza na wakuu wa Idara hiyo,wakiwemo ma-0fisa na wakaguzi wa elimu kutoka Halmashauri zote za mkoa huo,kilichofanyika mjini hapa.
Naibu waziri huyo aliwaambia watendaji hao kwamba uhaba na migomo ya walimu sio sababu za msingi kufanya vibaya kwa mkoa huo uendelee kuporomoka na kushika nafasi mwisho,kwani matatizo hayo yapo karibu nchi mzima.
“Tatizo la uhaba wa walimu lipo nchi nzima, migomo ya walimu pia imefanywa nchi nzima,ukiondoa baadhi ya maeneo machache tu,lakini wamefanya vizuri tafauti na mkoa wetu vipi”Alihoji Majaliwa.
Majaliwa akawaambia watendaji hao kwamba kufanya vibaya mkoa huo katika taaluma kunachangiwa zaidi na uongozi wa kutoshirikiana na walimu waliopo chini, kwa kujipanga na kujituma katika majukumu ya kiutendaji wa kila siku,ikiwemo kuingia madarasani na ufundishaji.
Naibu waziri huyo amewataka watendaji wa Idara hiyo,wakiwemo wale waliopelekwa kuhudumu mkoani Lindi,wanakuwa makini makini katika kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu yao,ili kuleta matokeo mazuri kwa siku zijazo kuanzia mwaka huu.
“Kama walimu ni wale wale waliopata mafunzo na kuuwezesha mkoa kushika nafasi za kwanza,pili na tatu kitaifa,kama ilivyokuwa mikoa mingine,kwa nini Lindi uwe chini zaidi,,,,,,,,nawaombeni sana mwaka huu wa 2013 na kuendelea uwe wa mabadiliko kwa mkoa wetu kufanya vizuri katika elimu zote za msingi na Sekondari”Alisisitiza Majaliwa.
Aidha amewaagiza viongozi wa idara hiyo,kutowaruhusu walimu kujihusisha na biashara kwenye maeneo ya Shule zao, na kwamba wale watakaokwenda kinyume na agizo hilo,wachukuliwe hatua za kisheria.

Pia amewasisitiza wakaguzi na waratibu elimu kata kuacha tabia ya kukaa ma-ofisini,badala yake wawafuatilie na kukagua hali ya elimu kwenye maeneo yao,ikiwa ni pamoja na kuona kazi zinazofanywa na walimu wao.
“Wakaguzi na waratibu elimu kata sio kazi yenu kushinda ma-ofisini,wote watembeleeni walimu,mkaone kazi wanazozifanya pamoja na kusikiliza matatizo yao”Alisisitiza Naibu waziri huyo.
Awali akiwasilisha taarifa katika kikao hicho, mshauri wa masuala ya elimu mkoani Lindi,Silas Samaluku,alisema ili kuodokana na tatizo hilo,mkoa unahitaji walimu wapatao 6,270 kwa Shule za msingi na Sekondari,lakini walipo ni 4,171 kati yao 3,338 wa Shule za msingi na 833 kwa Shule za Sekondari.
Hali ambayo alidai ni moja ya sababu zilizochangia kufanya vibaya katika mitihani yake elimu ya msingi na ile ya kidato cha pili kwa mwaka uliopita (2012).










About Author

Advertisement

 
Top