Christopher Lilai,Nachingwea
WANANCHI kukosa hamasa toka kwa viongozi wa siasa na wa serikali juu umuhimu wa elimu ya watu wazima kumetajwa kuwa ni kati ya sababu za kisomo hicho kutofanikiwa na kuongezeka kwa wasiojua kusoma na kuandika wilayani Nachingwea.
akizungumza na mtandao huu ofisini kwake afisa elimu ya watu wazima, kwa sasa wamekuwa wanasisitiza zaidi elimu ya msingi na kusahau elimu ya watu wazima ambayo ndio mama wa elimu zote na pia ni kiini cha maendeleo ya familia.
Risala hiyo ilitaja changamoto zingine zinazoikabili elimu ya watu wazima kuwa ni kukosekana kwa takwimu sahihi za watu wazima na vijana wenye umri lengwa wasiojua kusoma wala kuandika kutokana na baadhi yao kutokuwa tayari kujitokeza kutambuliwa kwa kuona aibu wakati wa sensa ya kila mwisho mwaka na pia baadhi ya watendaji na viongozi wa ngazi za vitongoji,vijiji na kata kutotoa ushirikiano wakati wa uendeshaji wa zoezi la sensa ya kubaini wananchi wasiojua kusoma na kuandika.
Changamoto nyingine ni suala la elimu ya watu wazima kuachiwa sekta ya elimu peke yake badala ya kila sekta iwe ya umma na binafsi kujihusisha kwa njia moja ama nyingine katika kutoa michango ya hali na mali katika kuboresha uendelezaji wa programu za elimu hii kwa ajili ya maendeleo ya familia na jamii kwa jumla.
Wilaya ya Nachingwea ina watu wazima na vijana 19,674 kati yao wanawake 10,939 na wanaume 8,305 ambao walibainika kutojua kusoma na kuandika kati ya watu wazima wote wapatao 89,305 sawa na asilimia 21.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.