Unknown Unknown Author
Title: SERIKALI (M) LINDI YASISITIZA USHIRIKIANO NA WALEMAVU.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Said Hamdani, Lindi. UONGOZI wa Serikali mkoani Lindi,umewahakikishia walemavu wote,utawajali, kuwathamini na kushirikiana na vyama vyo...

Na Said Hamdani, Lindi.
UONGOZI wa Serikali mkoani Lindi,umewahakikishia walemavu wote,utawajali, kuwathamini na kushirikiana na vyama vyote vya watu walio na ulemavu,ikiwemo kupunguza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabiri,ili kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Kauli hiyo imetolewa na jana na kaimu mkuu wa mkoa huo,Dk,Nassoro Himidi,alipokuwa akizungumza na walemavu wenye matatizo ya kusikia (Viziwi) wakati akifungua warsha inayoendeea kufanyika ukumbi wa Procure mjini Lindi.
Akifungua warsha hiyo ya siku tatu,yaliyoandaliwa na na Chama cha viziwi Tanzania (CHAVITA) tawi la Lindi,na kufadhiliwa na taasisi isiyo ya kiserikali,the Foundation Civil Society Ltd, Dk Himidi amewahakikishia walemavu hao kwamba Serikali ya mkoa huo,itaendelea kujenga mshikamano mzuri na vyama vyote vya walemavu bila ya ubaguzi.
Dk, Himidi ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo ya Lindi,amesema hakuna sababu za msingi kwa viongozi wa Serikali au vyama vya siasa na taasisi yeyote iwe ya umma ua watu binafsi kuwatenga au kuwanyanyapaa watu wenye matatizo ya ulemavu.
“Walemavu ni watu kama walivyo wengine ndani ya jamii zetu,hivyo sioni sababu wala kigezo cha kuwabagua kwani hawakupenda kuzaliwa wakiwa katika hali hiyo,ila ni mapenzi ya mwenyezi mungu mwenyewe”Alisema Dk,Himidi.
Pia amekiaidi kukipatia Chama hicho kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Shule itakayowasaidia kuwapatia Haki zao za msingi za kupata elimu itakayowawezesha katika kuendesha maisha yao ya baadae.

Aidha,kaimu mkuu huyo wa mkoa wa Lindi,amewaagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri na Manispaa wa mkoa huo,wawe na takwimu za watu wenye ulemavu ili kuiwezesha Serikali kuwa na mipango sahisahi inayohusu maendeleo na huduma muhimu kwa ajili ya walemavu.
Mwanzoni akimkaribisha kufungua warsha hiyo, mwenyekiti wa CHAVITA mkoani Lindi, Sultani Iqbral,alisema kukosa ushirikiano kati ya viongozi,baadhi ya jamii ni moja ya changamoto inayowakabiri walemavu.
Alisema matatizo mengi yanayotokea na yatakayoendelea kutokea yasipofanyiwa kazi,ikiwemo suala la Lugha ya alama kutaweza kusababisha uendelevu wa kutengwa na kubaguliwa na baadhi ya jamii iliyowengi.
Mafunzo hayo ya siku tatu na kufadhiliwa na the Foundation Civl Society Ltd, yameanza kufanyia Januari 22 hadi 24 mwaka huu,yamejumuisha washiriki wapatao 24 kati yao wanaume (14) na wanawake (10).








About Author

Advertisement

 
Top