Unknown Unknown Author
Title: Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete Atua Mkoani Arusha Nakufunga Mkutano wa Masuala ya Afya na Mtoto
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif...

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid (mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea  Arusha kwa ajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan. 17, 2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya  ngoma mbalimbali za utamaduni  alipowasili  katika  kiwanja  cha ndege cha Kimataifa cha Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani  Arusha.  Aliengozana nae  wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora ZeloteKikundi cha kinamama  cha ngoma ya Msanja  kikitumbuiza katika
mapokezi ya Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) Mama salma Kikwete (hayupo pichani)   kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro  (KIA) Jan 16,2013.Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO

About Author

Advertisement

 
Top