MISS TEMEKE ALIVYOPANIA KUMPOTEZA JACKLINE WOLPER KWENYE TASINIA YA FILAMU TANZANIA 2013!

Mafanikio yoyote huja kwa mipangilia na maandalizi.Hivyo ndivyo ninavyoweza kumzungumzia Irene Kanka "19" ambae aliwahi kuwa mshindi namba nne kwenye kinyang'anyilo cha kumtafua Miss Temeke 2011.
Irene ambae ni mtoto wa tatu kati ya watoto watano kwenye familia ya mzee Kanka inayoiishi Singida.Mrembo huyo kwa sasa anaongoza kupiga mkwanja mrefu kwenye dili za matangazo kwenye mitandao mikubwa kama Voda Com,Tigo na Airtel na kampuni nyinginezo.
Irine licha ya kupiga bao kazi hiyo ya kuuza sura kwenye matangazo lakini pia amemudu vyema kuigiza hali inayowatia hofu mastaa wakubwa kwenye fani hiyo.
Mrembo huyo ameonesha maajabu kwenye filamu ya June 26 kiasi cha kuwachanganya "Directors" na kumtabilia nyota njema 2013 kuwa huenda akawafunika mastaa wa kike kama Jackline Wolper,Irene Uwoya,Wema Sepetu na wengineo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post