Unknown Unknown Author
Title: KIKONGWE ATOA TAMKO: BOMBA LA GESI KUSAFIRISHA MAJI KAMA WAKIMPINGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KIKONGWE Somoe Issa anayekadriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 90 ambaye ni Mkuu wa Kaya ya Msimbati kijiji ambacho gesi asilia inavunwa, m...
Bibi Somoe Issa kushoto, kulia ni mwanidhsi wa habari wa info radio mjini Mtwara.KIKONGWE Somoe Issa anayekadriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 90 ambaye ni Mkuu wa Kaya ya Msimbati kijiji ambacho gesi asilia inavunwa, mkoani Mtwara ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake mwishoni mwa wiki, kikongwe huyo ambaye haoni na hasikii vizuri alisema hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji chake ambacho ni urithi kutoka kwa wazee wake ikiondoka mkoani Mtwara
“Atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakachomkuta atakijua yeye mweyewe…ninasema gesi isiende kokote…iwapo atabisha inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewe” alisema bibi huyo kupitia kwa mkalimani wake Asha Hamis
Aliongeza kuwa “Mwaka walioanza kuchimba (2005) walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta…bomba lilikuwa haiendi chini wala kurudi juu…walinifuata hapa nikaenda kufanya tambiko”
Katika maongezi yake na waandishi wa habari bibi huyo alilazimika kutumia lugha ya kimakonde kwa maelezo ndiyo anayoifahamu vizuri, alisema wakati wa tambiko hilo wazungu waliokuwa katika mradi huo walilazimika kunywa maji kwa kutumia kifuu cha nazi ambapo mmoja wao alikataa.

“Yule aliyekataa niliwaambia aondoke, wale wenzake walimsafirisha na baada ya hapo waliaza kuchimba na gesi ikapatika…leo wanasema gesi inaondoka, hilo sikubali…mimi ndiye mwenye eneo hili, nilifanya tambiko gesi ipatikane na sasa nitafanya tambiko isiondoke” alisisitiza kikongwe huyo ambaye hajui mwaka aliozaliwa.
Kauli ya Kikongwe huyo kupinga gesi kwenda Dar es Salaam na kutishia kusafirishwa kwa maji badala ya gesi iwapo serikali itapuuza madai ya wananchi inarejesha historia ya vita ya Majimaji iliyoasisiwa wilayani Kilwa, mkoani Lindi mwaka 1905-7.
Katika vita hiyo viongozi wa kimila walisema kuwa bunduki za wazungu zitatoa maji badala ya risasi, jambo ambalo lilihamsisha wananchi wengi kupigana vita hivyo.
Kwa kauli hiyo ya mkuu huyo wa kaya anaungana na wakazi wengi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga mradi huo, wakiwemo wanasiasa, viongozi wa dini, mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji na CCM wilaya ya Mtwara mjini.
Tayari serikali imetoa msimao wake juu ya sula hilo kwa maelezo kwamba ni lazima mradi huo kutekelezwa kwa maslahi ya Taifa na kwamba wakazi wa Mtwara watafaidika nao.







About Author

Advertisement

 
Top