Unknown Unknown Author
Title: WANAHABARI TUMIENI KARAMU ZENU JUU YA BIDHAA BANDIA–YUSSUFU MATUMBO, MTWARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Mwandishi Wetu: Ahmeid A. Aziz WAANDISHI wa habari kanda wa kusini, inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara,wametakiwa kutumia vyema k...
clip_image002Na. Mwandishi Wetu: Ahmeid A. Aziz
WAANDISHI wa habari kanda wa kusini, inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara,wametakiwa kutumia vyema karamu zao kwa kuandika na kusambaza taarifa mbalimbali kwa jamii, juu ya kuenea kwa bidhaa bandia zinazotengenezwa na kuingizwa nchini, na baadhi ya wafanyabiashara wasiojari maisha na usalama wateja wao.
Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara,Yusufu Matumbo,ametoa rai hiyo,alipokuwa akifungua semina kwa waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wa mikoa hiyo,kwenye ukumbi wa Bandari Club mjini Mtwara
Semina hiyo ya siku moja iliandaliwa na mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) ilijumuisha washiriki zaidi ya (50) kutoka katika mikoa hiyo ya Mtwara na Lindi.
Akifungua semina hiyo,katibu tawala huyo akasema mamlaka ya Chakula na Dawa pekee haiwezi kutekeleza vyema majukumu yake kwa ufanisi bila ya kuwepo kwa ushirikiano na vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini,ili kuhakikisha kazi ya kuelimisha wananchi juu ya matatizo yanayohusiana usalama na ubora wa bidhaa kama Sheria namba (1) ya mwaka 2003 inayohusu Chakula, Dawa na vipodozi inavyotekelezwa.
Matumbo amesema kazi ya kupambana na vitendo vya uuzwaji na usambazaji wa bidhaa bandia zisizo na ubora hapa nchini sio rahisi kwa watu wachache kushinda vita hivyo, kunahitaji  ushirikiano wa karibu kati ya waandishi wa habari, Mamlaka husika (TFDA) na Jamiii kwa ujumla.
“Kwa kuzingatia umuhimu wenu wana habari na vyombo vyenu pamoja na michango mnayoitoa kwa Jamii ndio maana leo hii tumekutana hapa Leo kujadiliana kwa pamoja na kutoa maoni yatakayosaidia TFDA kuboresha huduma zake,,,,,,,Ili kulinda afya za watumiaji wa bidhaa zinazoingizwa nchini”Alisema Matumbo.
Akasema mamlaka ya Chakula na dawa wakifanya kazi kwa kushirikisha waandishi na vyombo vya habari,kwa kiwango kikubwa wananchi wataweza kuelewa matatizo yaliyopo katika Jamii yanayohusiana na usalama na ubora wa bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA, hali itakayosaidia kuhakikisha Sheria ya Chakula,Dawa na vipodozi ya mwaka 2003 inatekelezwa kwa ufanisi na wadau wote.

Matumbo amesema bidhaa za Chakula.dawa, vipodozi na vifaa tiba ni nyeti  na madhara yake ni makubwa kama hazikudhibitiwa ipasavyo,yanaweza kusababisha ulemavu,kupoteza maisha ya watu,ikiwa ni pamoja na kudhoofisha uchumi wa Taifa.
Akasema mfumo mzuri wa kudhibiti bidhaa bandia,ikiwemo Chakula dawa, vipodozi na vifaa tiba, unahitaji kuwa na Sheria madhubuti, utawala bora,na watalamu wenye ari na sifa ya kufanya kazi na miundombinu mizuri,ili kuzuia madhara kwa watumiaji.
Katibu tawala huyo akasema ili kufikia malengo halisi hapana budi kwa bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nchini,zinahitaji kufanyiwa uhakiki wa usalama,ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa kutumika,kazi ambayo inasimamiwa na TFDA.
Awali akimkaribisha katibu tawala kufungua mafunzo hayo,mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Hiiti Sillo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia waandishi na wahariri wa vyombo vya habari,wafahamu na kutekeleza majukumu na makubaliano ili kuwapatia elimu juu ya madhara ya bidhaa bandia kwa wananchi wa mikoa hiyo.
Sillo alisema kupitia kwenye vyombo vya habari,elimu hiyo inaweza kuwafikia wananchi waliowengi na kwa wakati mmoja na waweze kufanya maamuzi sahihi,wakati wa kuchagua bidhaa zinazowafaa kwa matumizi yao.
Katika semina hiyo,takribani mada tano zilifundishwa,ikiwemo Sheria ya Chakula,Dawa,vipodozi na vifaa tiba, bidhaa duni na bandia pamoja na changamoto zilizopo katika kuzitambua na udhibiti wake.
MKUU wa wilaya ya Nachingwea,mkoani Lindi,Regina Chonjo,amewataka vijana kushirikli katika mafunzo ya ulinzi, yakiwemo ya Jeshi la mgambo,ili yaweze kuwasaidia kujilinda na kujipatia ajira kupitia mfumo huo,kwa ajili ya kuendeleza maisha yao.
Rai hiyo ameitoa juzi wakati akifunga mafunzo ya miezi sita kwa wanamgambo 99 wa kata ya Naipanga,wilayani humo.
Chonjo akifunga mafunzo hayo, amewataka wahitimu hao,kuyatumia mafunzo ya ujasili waliyoyapata kwa kujilinda wao wenyewe pamoja na wananchi wengine na mali zao katika maeneo yao.
“Mafunzo mliyayapata ni ya ujasiri mkubwa kwani yanahusu utumiaji wa siraha na mbinu mbalimbali za kujilinda,,,,,,,,,hivyo mbinu hizo zisitumike kinyume na maadili yake” Alisisitiza Chonjo.
Akasema wakati waasisi wa Taifa hili wanaanzisha utaratibu huo miaka (41) iliyopita chini ya hayati mwalimu Julius Kamabarage Nyerere,yamelenga kuwapa wananchi mbinu za kujilinda na maadui wao na taifa kwa ujumla.
Mkuu huyo wa wilaya ya Nachingwea akasema iwapo mafunzo waliyoyapata watayatumia vibaya,ikiwemo kuhatarisha usalama wa watu wengine wasio na hatia na mali zao,watakuwa wamekwenda kiunyume na maana nzima ya maudhui yake.
Chonjo amesema kutokana na nchi ya Tanzania kuwa ya amani na utulivu mkubwa hivyo ni vyema kwa vijana wote wenye uwezo wa kufanya kazi katika wilaya hiyo,wakajiunga na mafunzo ya ulinzi ili wakaendeleza amana walivyotuachia waassisi wa Taifa letu.
Kiongozi huyo wa wilaya amewasisitiza pia wananchi kuendelea kuandaa mashamba yao,na kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa kwa kupanda mazao kwenye mashamba yao.
Awali wakila kiapo cha utii mbele ya mgeni rasmi,wanamgambo hao walisema mafunzo waliyoyapata watayatumia vizuri kwa kulinda usalama wa watu na mali zao pamoja na kuendeleza amani na upendo kwenye maeneo yao wanayoishi na wilaya kwa ujumla.
Mafunzo hayo ya miezi sita yalianza mwishoni mwa mwezi mei 2012 na kumalizika Decemba mwaka huu,yameshirikisha wanamgambo wapatao 99 kutoka vijiji viwili kati ya vine vilivyopo kata hiyo ya Naipanga.






















About Author

Advertisement

 
Top