TFF MUMEIPATA HII?: SUPERSPORT HAWALIPI SENTI TANO NYEKUNDU CECAFA KURUSHA CHALLENGE

TELEVISHENI ya kulipia ya kimataifa, SuperSport ya Afrika Kusini inarusha mashindano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Tusker Challenge bila kulipia chochote, imeelezwa.

Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alisema jana kwamba, wameamua kuwapa haki ya kurusha matangazo SuperSport bila malipo, ili kuitangaza soka ya ukanda huu.

“Watu wamekuwa wakilalamika sana kwamba mashindano ya CECAFA hayaonekani kwenye TV, sasa sisi tukaamua kuwapa haki hiyo bure SuperSport ili kupromoti soka yetu, je ni vibaya?”alihoji Musonye.

Pamoja na SuperSport kurusha matangazo hayo bure, Musonye ameondoa dhana kwamba, Televisheni nyingine za nchi za CECAFA zinazuiwa kurusha matangazo hayo.

“Hakuna TV ambayo inazuiwa, Tanzania TBC huwa wanaonyesham Kenya KBC huwa wanaonyesha na Uganda pia UBC wanaonyesha, hatuzuii sisi TV kurusha matangazo yetu,”alisema Musonye.

Wakati SuperSport ikirusha bure matangazo ya mashindano ya CECAFA, nchini Tanzania Kamati ya Ligi Kuu inazuia Vituo vya Redio na Televisheni kurusha bure mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na hivi sasa kuna mgogoro mkubwa baina ya pande hizo mbili.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post