Mkurugenzi wa Tahmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ambapo amesema Wizara imetoa agizo la kufanya ziara katika Viwanda vilivyopo eneo la Mikocheni na fukwe za hoteli zilizoko katika bahari ya Hindi maeneo ya Manispaa ya Kinondoni kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo ambayo huleta athari kwa jamii kwa ujumla. Katikati ni Mkuu wa Msafara Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na kulia ni Mkemia Mkuu wa Mazingira katika Ofisi hiyo Bi. Rogathe Kisanga.Mkurugenzi wa Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga kutoka NEMC akitoa maelezo kwa Naibu Waziri ambapo amesema NEMC imetoa agizo kwa wamiliki wa Viwanda kuhakikisha wanafunga mitambo maalum yakusafisha maji taka yatokanayo na bidhaa wanazozitengeneza hasa zinazotumia rangi kabla ya kuyamwaga katika mifumo ya maji machafu ili kupunguza athari za uharibu wa mazingira.Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri kuhusiana na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kisheria kwa watu wanaochafua mazingira wakiwemo wanaomwaga maji machafu yenye kemikali zinazoharibu Mazingira kutoka viwandani wakati wa ziara ya kukagua Mto Mlalakuwa uliopo maeneo ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Huu ndio Mto Mlalakuwa Kawe Darajani unavyoonekana ambapo maji yake yanaonyesha kuchafuliwa na maji taka yatokayo viwandani.Pichani Juu na chini ni Mheshimiwa Naibu Waziri Charles Kitwanga (katikati) kipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kuratibu Miradi wa kiwanda cha MM I Steel Bw. Lawrance Manyama (kushoto) wakati alipofanya ziara rasmi kuangalia changamoto za uharibu wa mazingira unaotokana na Viwanda na Mahoteli. Kulia ni Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga.Mh. Charles Kitwanga akikemea vikali tabia ya uchelewashwaji wa maagizo yanayotolewa na Serikali wakati wa ziara yake katika Kiwanda hicho sambamba na viongozi wa NEMC.Naibu Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha awamu ya kwanza ya ziara ya kutembelea viwanda vya jijini Dar es Salaam ambapo amesema ziara hiyo imempa nafasi ya kujionea hali halisa ya viwanda vya jijini na kugundua kuwa vingi havina mitambo ya kusafisha maji machafu yanayokwenda kumwagwa kwenye mito na kushuhudia kuwa vingine havina viwango vya kupeleka maji taka yake kwenye mtandao wa maji taka ya DAWASCO na kuwataka kufikia viwango vinayokubalika na mazingira yetu.
Home
»
DAR ES SALAAM
» MH. CHARLES KITWANGA AFANYA ZIARA YA GHAFLA KATIKA VIWANDA JIJINI DAR ES SALAAM
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.