Ashley Cole wa Chelsea (kulia) akiruka kumkabili mchezaji wa timu ya Corianthians, Jorge Enrique wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu uliochezwa Yokohama leo.
Klabu ya Corrinthians kutoka Brazil, imeshinda kombe la klabu bingwa duniani baada ya kuilaza Chelsea bao moja kwa bila katika mechi ya fainali iliyochezwa nchini Japan.
Paolo Guerrero aliifungia Corinthians, bao hilo muhimu na la ushindi.
Hata hivyo Chelsea, ilipoteza bafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo.
Katika muda wa ziada Fernando Torres, alipoteza nafasi nzuri sana ya kusawazisha licha ya kuwapiku walinzi wa Corinthians na kubakia kipa pekee.
Torres alijaribu kumchenga kipa wa Corinthians lakini kombora lake likawa hafifu na kudakwa kwa urahisi na kipa.
Chelsea ilimaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji kumi baada ya Gary Cahil, kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Corrinthians Emerson.
Bao la chelsea lililofuingwa kwa kichwa na Fernando torres lilikataliwa na hivyo vijana hao kutoka brazil wakaibuka na ushindi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.