Amir Khan amzidi Carlos Molina

Amir Khan Katika ndondi baada ya kushindwa mapigano mawili mfululizo, Amir Khan wa Uingereza amemshinda Carlos Molina, katika pambano lililoandaliwa mjini Los angeles.

Khan, mwenye umri wa miaka 26, alipoteza mataji yake ya WBA na IBF katika uzani wa light-welterweight baada ya kushindwa na Danny Garcia na Lamont Peterson.

Lakini katika pigano hilo lililofanyika jana usiku, Khan alimuadhibu Molina kiasi cha kumlazimisha muamuzi wa pambano hilo kuisimamishwa katika raundi ya kumi ili kumuokoa Molina.

Ushindi huo ndio wa kwanza kwa Khan, ambaye kwa sasa anapewa mafunzo na Virgil Hunter na huenda akaamua kupambana na Garcia au Peterson, kujaribu kurejesha mataji yake, aliyoyapoteza.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post