Mwakilishi wa taasisi ya Molly’s inayojihusisha na utoaji misaada kwa taasisi za kijamii Catharine Paul Hiicks (watatu kushoto) akimkabidhi cheki yenye thamani ya Dola za kimarekani 2369/ Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania Angela Kuzilwa, mara baada ya kukabidhi msaada wa matiti bandia na sidiria maalum kwaajili ya waliokatwa matiti vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 10Millioni jijini Dar es Salaam leo.Wafanyakazi wa Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania na baadhi ya wanachama wa taasisi hiyo wakiinua juu moja ya maboksi yenye matiti bandia na sidiria maalum kwaajili ya watu waliokatwa matiti mara baada ya kukabidhiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Molly’s Catharine Paul Hicks vyenye thamani ya zaidi ya Dola 10Millioni jijini Dar es Salaam leo.
Akina mama hao wakiwa wameshika matiti bandia na sidiria maalum walizokabidhiwa.ASASI ya Saratani ya Matiti Tanzania leo imepokea Msaada wa matiti bandia na sidiria maalum kwaajili ya waliokatwa matiti pamoja na msaada wa cheki ya pesa , vyenye thamani ya zaidi ya Millioni 12.
Akizungumza na Mtandao huu mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo na Cheki Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Angela Kuzilwa, alisema wamekabidhiwa msaada wa matiti bandia yapatayo 30 na sidiria maalumu zipatazo 30, pamoja na Cheki yenye thamani ya Dola za Kimarekani 2369 kutoka kwa taasisi ya Molly’s inayojihusisha na utoaji wa misada ya kjamii.
Kuzilwa aliuambia mtandao huu kuwa wamekua na changamoto nyingi kwenye taasisi hiyo ambazo pekeyao hawataweza kuzikabili bila kupata misaada kutoka kwa taasisi na mashirika mbalimbali pamoja na Serikali.
Pamoja na kuishukuru taasisi ya Molly’s Kuzilwa amesema vifaa bandia kwa waathirika wasaratani ni ghali sana kiasi kwamba mtanzania wakawaida ni vigumu kuweza kumudu kununua ambapo alitoa mfano wa titi moja bandia linafikia thamani ya Tsh 300,000/ (laki tatu).
Nae mwakilishi wa Taasisi ya Molly’s alisema taasisi yao iliwatembelea na kuzungumza nao viongozi wa taasisi hiyo ilikujua Changamoto zinazowakabili ndipo walipogundua tatizo hilo na kuwatafutia fedha za kununua vifaa hivyo kutoka kwa wahisani wengini nchini Uingereza.
Asasi ya Saratani Tanzania ilianzishwa mwaka 2008 ili kuweza kuunganisha nguvu kwa walioathirika saratani na kuweza kuweza kuwasaidia wengine wanahisi dalili zakuwa na saratani ambapo hadi hivio sasa wanawanachama zaidi ya 370.