NIJUZE NIJUZE Author
Title: WAANDISH NA WANA ASASI WAPIGWA MSASA KUHUSIANA NA HAKI YA KUPATA HABARI NA KUCHANGIA UWEPO WA VIPENGELE VYA KATIBA MPYA NCHINI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Washiriki wa Mafunzo kuhusiana sheria ya haki ya kupata habari Mwandishi mwandamizi,Attilo Tagalile akitoa mada katika mafunzo hayo ya ...
Washiriki wa Mafunzo kuhusiana sheria ya haki ya kupata habari
Mwandishi mwandamizi,Attilo Tagalile akitoa mada katika mafunzo hayo ya siku 2 yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam

Waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa Asasi zisizo za kiserikali toka mikoa ya Lindi,Mtwara,Pwani na Dar wanapata mafunzo ya siku 2 kuhusiana na sheria ya haki ya kupata habari pamoja na sheria ya huduma ya vyombo  katika vya habari ili kuchangia uwepo wa vipengele vipya katika katiba ijayo,
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania yana lengo la kuwaandaa wanahabari na wadau kujipanga na kutambua wajibu na umuhimu wao  katika kuchangia na kuelimisha wanajamii kuchangia maoni yao ili kupata haki ya kikatiba kuchangia maendeleo Nchini,


Akizungumza katika mafunzo hayo,Mwandishi wa Habari mwandamizi Nchini,Attilio Tagalile ameeleza kuwa wanahabari wanahabari wanatakiwa kutumia fursa ili kupitisha ajenda za wanahabari na vyombo vya habari
katika katiba Ijayo,


Aidha aliwataka kufuata sheria na kanuni za kufuatia sheria zilizopo kuwabana wanahabari kufanya kazi zao ambapo taasisi binafsi na za umma bila vikwazo.

HABARI NA: Abdulaziz video.Dar

About Author

Advertisement

 
Top