NIJUZE NIJUZE Author
Title: Msaada wa Matibabu kwa mama huyu alie wilayani Ruangwa unahitajika afike Muhimbili kwa Matibabu zaidi
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Bi Arafa Issa Namaji(Pichani) mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji  cha Narung’ombe wilayani Ruangwa Mkoani Lindi  anaomba msaada wa  ...

Bi Arafa Issa Namaji(Pichani) mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji cha Narung’ombe wilayani Ruangwa Mkoani Lindi  anaomba msaada wa haraka utakaomuwezesha kupata matibabu ya uvimbe ulio katika paji la uso uliotokana na maumivu makali ya kichwa baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Ndanda na kuelekezwa kufika katika hospital ya Taifa ya Muhimbili(MNH) Kwa uchunguzi zaidi na matibabu. Tatizo lilianza tangu mwezi february 2012,alianza kwa kuumwa na kichwakwa maumivu makali sana na kipele kidogo kikatokea kwenye paji
la uso,hivyo basi kadri kilipopungua maumivu ndipo kipele kiliendelea kuwa kikubwa hadi kuathiri macho na sehemu ya pua baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya Majirani na marafiki wa karibu walimshauri kwenda hospitali ya wilaya, alipofika Daktari  alimpa rufaa ya kwenda hopsitali ya Ndanda,hata hivyo Ndanda pia wakampa rufaa kwenda hospitali ya rufaa muhimbili kwa uchunguzi zaidi.kutokana na hali hiyo ngumu aliyonayo
Kutokana na kuwa katika hali duni na hana mtu yeyote wa kumsaidia Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wameichangishana kupata kiasi cha nauli pamoja na hela kidogo ya kujikimu kwa siku mbili,lakini bado anahitaji msaada zaidi wa pesa kwasababu atahitaji kuishi zaidi DSM Akiwa  katika hospital ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu yake Kwa alietayari kumsaidia anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid kwa namba za simu
0787176221 au 0756696048 

Kutoa ni Moyo ili kumsaidia mama huyu

About Author

Advertisement

 
Top