Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa akifungua mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika leo Oktoba 20, 2012 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muhula uliopita, Waziri Sophia Simba amefanikiwa kukitetea kiti hicho, kufuatia duru za uchaguzi mkuu wa Jumuia hiyo uliofanyika leo mjini Dodoma, kuonyesha kuwa ameshinda.
Habari zinasema, katika uchaguzi huo uliosimamiwa na viongozi mahiri akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Wilison Mukama na Mjumbe wa NEC wa zamani Abdulrahman Kinana, Simba ametajwa kuongoza kwa kura nyingi dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Anne Kilango Malecela. TUTAWALETEA MATOKEO KAMILI TUKIYAPATA.