Baada ya Toto Africa kuendelea kumpa wakati mbaya kocha wa JKT Ruvu Charles Kilinda, kesho (oktoba 10) watakuwa na kibarua mbele ya vijana wa Abdallah King Kibaden, Kagera Sugar katika uwanja wenye kumbukumbu mbaya kwa vigogo, uwanja wa Kaitaba. JKT Ruvu wameteremka uwanjani mara 6 na kupoteza michezo 4 huku wakishinda miwili dhidi ya timu za jeshi la kujenga Taifa, Ruvu Shooting na Mgambo Shooting ya Tanga.
JKT Ruvu ikiwa ndio timu iliyoruhusu magoli mengi katika nyavu zao wamefungwa na Simba SC, Yanga SC, Azam FC na Toto Africa ya Mwanza.
Kagera Sugar ambao wako katika nafasi ya 3 kwa kufikisha point 10 baada ya kushuka uwanjani mara 6 wakishinda michezo mitatu wakitoka sare mmoja dhidi ya JKT Oljoro katika uwanja wa Kaitaba na wakipoteza miwili dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Kaitaba na Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani.
Vijana hao wananolewa na Kibaden watakuwa na kazi ya kuendeleza ushindi wao mbele ya JKT Ruvu ambapo mara nyingi wanapokutana katika uwanja wa Kaitaba mchezo humalizika kwa matokeo ya Sare.
Tags
MICHEZO