Unknown Unknown Author
Title: FALCON, JAMHURI ZAJITOA MICHUANO YA CAF!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wawakilishi wa Zanzibar katika Michuano ya Kimataifa kwa ngazi ya vilabu wamejitoa katika michuano hiyo. Habari zilizopatikana na kuthibitis...

Wawakilishi wa Zanzibar katika Michuano ya Kimataifa kwa ngazi ya vilabu wamejitoa katika michuano hiyo.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Rais wa Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar (Zfa), Aman Ibrahim Makungu, ni kuwa timu ya Super Falcon ambao ni mabingwa watetezi katika ligi kuu ya Zanzibar, ambao walikuwa waiwakilishe Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mwakani pamoja na timu ya Jamhuri ambao ni makamo bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar na ambao walikuwa waiwakilishe Zanzibar katika kombe la shirikisho hapo mwakani kwa pamoja wameamua kujitoa katika michuano hiyo.
Chanzo cha timu hizo kujitoa inasemekana ni ukata wa fedha, ambapo kila timu ilihitaji dola 30,000 kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki wa michuano hiyo.
Kufuatia hatua hiyo chama cha soka visiwani Zanzibar, kiko katika mazungumzo na baadhi ya vilabu vya ligi kuu ili kuona kama kuna uwezekano wa kupata timu zitakayochukua nafasi hizo.
Mwaka huu Zanzibar iliwakilishwa na timu ya Mafunzo katika ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku Jamhuri wakipata nafasi ya kushirki katika kombe la Shirikisho.
Hata hivyo timu zote zilishindwa kufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya mwanzo katika michuano hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top