Babu Mtopa atetea kiti chake licha ya kuwa na tishio la kuangushwa madarakani na kundi la Vijana

image Ally Hassan Gwaja Mgombea aliengushwa na Babu Mtopa  jana katika ukumbi wa Yongolo Ruangwaimage Wajumbe wa CCM Wilaya Nachingwea wakiongozwa na Mwenyekiti wa ccm wilaya Bw ALBERT Mnali(Kiboko ya Walimu)Na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Regina Chonjo
Na. Abdulaziz,Lindi

image MWENYEKITI wa wenyeviti wa CCM wa mikoa yote Nchini ambae pia ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi ,Alli Mohamedi Mtopa amefanikiwa kutetea nafasi yake baada ya Upinzani Mkali alioupata toka kwa Mpinzani wake
Katika Uchaguzi huo chama hicho Mkoani Lindi,Mzee Mtopa(85)alifanikiwa kutetea kiti hicho kwa kipindi cha Tatu baada ya kumshinda mpinzani ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lindi Vijijini,Bw Ali Hassan Gwaja katika Uchaguzi ambao umefanyika huku kukiwa na mabadiliko makubwa ya uongozi wa Chama katika Chaguzi ngazi za wilaya
Akitangaza matokeo hayo katika Mkutano mkuu wa Uchaguzi mkoa wa Lindi,Mwenyekiti wa Muda wa Uchaguzi huo,Murtaza Mangungu,Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini alimtangaza Mshindi baada ya kujinyakulia kura 523 Kati ya 838 zilizopigwa huku Mpinzani wake akiambulia kura 314 huku kura moja ikiharibika.
image
Akifunga Mkutano huo baada ya kumalizika kwa chaguzi mbalimbali kukamilisha Safu ya Uongozi wa CCM Mkoa wa Lindi,Msimamizi mkuu wa Uchaguzi huo,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ,Ambae pia ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ,Bernard Membe aliwataka wana CCM kushikana na kusisitiza kuwa Kuangushwa kwa chama Tawala hakutokani na Wapinzani bali kunachangiwa ndani ya Chama hicho
Licha ya Ushindi huo,akishukuru wapiga kura Mzee Mtopa alikiri kuwepo kwa Upinzani mkubwa dhidi yake na kueleza kuwa Ushindi wake unatoka na Hekima,Maarifa aliyonayo huku akieleza alivyojipanga kuongoza chama hicho katika kipindi kijacho
image
Katika Uchaguzi huo nafasi ya katibu wa Uenezi wa mkoa ilinyakuliwa na Ibrahimu Said Mpwapwa ambaye alifanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata kura za ndio baada ya nafasi hiyo kukosa mpinzani,huku Nafasi ya Katibu wa uchumi na fedha Ilitetewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi, Frank Raphael Magali ambaye aliwashinda Mohamed Lidume Lihumbo na Rashidi Hasani Nakumbya.













Previous Post Next Post