Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WILAYANI KILWA WAOMBWA KUJITOKEZA KESHO KATIKA MDAHALO WA KUJENGA UELEWA WA JINSI YA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Zikiwa zimebaki siku chache kufikiwa na Tume ya Ukusanyaji wa Maoni ya Mchakato wa Katiba mpya inayoendelea Mkoani Lindi, Wananchi wa Wilay...
image Zikiwa zimebaki siku chache kufikiwa na Tume ya Ukusanyaji wa Maoni ya Mchakato wa Katiba mpya inayoendelea Mkoani Lindi, Wananchi wa Wilayani Kilwa Wameombwa kuhudhuria katika mdahalo wa Uhamasishaji na kujenga uelewa juu ya Utoaji wa Maoni Yao
Mdahalo huo Utakaofanyika katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo Wilayani Humo ambao umeandaliwa na Mtandao wa Asasi zisizo za kiserikali wilayani Kilwa na Kufadhiliwa na The Foundation for civil society ni harakati za kuongeza ushiriki wa Jamii ikiwemo wa Vyama vya siasa,Taasisi za Dini,Halmashauri ,Wazee wakiwemo vijana katika mchakato wa kupata katiba mpya TANZANIA
Asasi ya Kingonet itafanya mdahalo kesho Jumatatu tarehe 10 na kuanza saa 3 asubuhi

Akizungumza na blogu hii,Katibu wa Kingonet,Bw Omary Mkuwili alieleza kuwa Asasi yake ina lengo la kuwajengea Uelewa ili Jamii wilayani humo kutumia Fursa hiyo kushiriki kwa ukamilifu na kutoa maoni yatakayosaidia jamii kuishi na kufuata katiba ambayo itakuwa ya kwanza kutungwa na Watanzania wenyewe kufuatia maoni yao watakayoyatoa
‘’Nawaomba wana Kilwa kutumia fursa hii na kujitokeza kwa wingi kesho ili kupata fursa ya kuelewa na kujengewa uwezo wa jinsi ya kutoa maoni yao kabla Tume haijafika wilayani Kilwa hii ni fursa pekee iliyotolewa na Kingonet kupitia The Foundation Ni nafasi adimu Tuitumie kwa Maendeleo ya Kilwa na Tanzania…..Alimalizia Mkuwili
Tume ya Maoni ya Katiba ikiongozwa na Mama Salama Kombo Ahmeid ipo Mkoani Lindi tokea tarehe 28/08/2012 ambapo ilianza katika wilaya ya Liwale,Nachingwea na sasa wapo katika Wilaya Ruangwa
Kwa Wilaya ya Kilwa Tume hiyo itaanza kazi zake tarehe 24 ya mwezi huu.
Na Abdulaziz Video,Kilwa Masoko






About Author

Advertisement

 
Top