Unknown Unknown Author
Title: VIONGOZI WA HALMASHAURI ZA LINDI WAHAMASIHSWA MATUMIZI YA MADINI JOTO KATIKA ZAO LA CHUMVI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nassor Hamid akihutubia hadhira ya wajumbe walio hudhuria kikao hicho. Madini joto yawekwayo katika chumvi ...
image Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nassor Hamid akihutubia hadhira ya wajumbe walio hudhuria kikao hicho.
Madini joto yawekwayo katika chumvi ni nyongeza lishe ya madini ya aina ya iodine, ambayo ni madini muhimu katika ukuaji wa akili na ufahamu wa mtu mzima na mtoto katika hatua zote za ukuaji kuanzia tumboni kwa mama. Pia ni madini yanayozuia ugonjwa wa tezi la shingo (Goitre) linalosababishwa na upungufu wa madini hayo katika mwili. Madini haya yanapatikana ardhini na katika vyakula vinavyomea katika ardhi hiyo. Hata hivyo, pamoja na kupatikana katika ardhi, tafiti zinaonesha kwamba kutokana na uharibifu wa mazingira na kwa sababu za kijografia, maeneo mbalimbali yameonekana kuwa na upungufu mkubwa wa madini hayo. Pia inakadiriwa kwamba 41% ya Watanzania wanaishi katika maeneo yenye upungufu wa madini hayo, na asilimia 25% wameathirika na upungufu wa madini hayo nchi nzima (URT, 1980-1990)
image Moja ya maeneo yanayosadikika kuathirika zaidi ni maeneo yote ya mwinuko ambayo kutokana na mbinu hafifu za kilimo, n.k tabaka la juu lenye madini hayo linachukuliwa na kwenda katika maeneo ya tambarare, baharini, maziwa na kadhalika. Kwa mukitadha huu shirika la afya duniani lililazimika kutafuta njia rahisi na ya gharama nafuu kufidia upungufu huu, na kwa maazimio inaonekana chumvi ndiyo kiungo ambacho kila mtu anaweza kununua na ndiyo kiungo pia ambacho watu walio wengi dunia wanatumia katika maisha yao ya kila siku.
Katika Mikoa ya kusini (Lindi na Mtwara) tafiti zinaonesha kwamba chini ya 50% ya kaya zinatumia chumvi isiyo na madini joto.Kutokana na tafiti matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa mkoa wa Lindi ni asilimia 25 tu ya kaya zote. Hata hivyo tathmini ya matumizi ya chumvi yenye madini joto katika halmashauri ya wilaya ya Lindi iliyofanyika katika tarafa mbili za Nyangamara na Milola katika mwaka wa 2011/2012 zaidi 50% ya kaya zina uelewa wa madini joto na zinatumia chumvi yenye madini joto.imageHALI ILIVYO SASA
Mkoa wa Lindi ni wa mwisho kwa matumizi ya chumvi yenye madini joto ingawa ni moja ya mkoa unaoongoza kwa kuzalisha chumvi nyingi. Mkoa wa Lindi una 6% tu ya kaya zinazotumia chumvi yenye madini joto. Kitaifa ni 82% ya kaya katika Tanzania ndizo zinatumia chumvi yenye madini joto.

Moja ya mikakati iliyowekwa katika kikao hiki ni kuwakamata wauzaji wote wa chumvi isiyo na madini joto, kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya madini joto, Gharama za kununua madini joto zipunguzwe ili kuwafanya wazalishaji wadogo kuweza kununua madini hayo.


Kumbuka: Chumvi inayotiwa madini joto kwa wazalishaji Lindi inasafirishwa kwenda mikoa ya wenzetu na wenyewe kuuziana chumvi isiyo na madini joto.
HABARI NA PICHA : LIMWAGU ELVAN





About Author

Advertisement

 
Top