Unknown Unknown Author
Title: UEFA CHAMPIONZ LIGI: MECHI DEI 2 Jumanne & Jumatano!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
>>MVUTO: Benfica v FC Barcelona, Ajax v Real, Man City v Borussia Dortmund!! Timu 32 zinawania kutinga Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LI...
>>MVUTO: Benfica v FC Barcelona, Ajax v Real, Man City v Borussia Dortmund!!
UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZTimu 32 zinawania kutinga Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Uwanjani Wembley Jijini London hapo Tarehe 25 Mei 2013 na tayari Timu hizo zishamaliza ‘Mechi Dei 1’, yaani wameshacheza Mechi zao za kwanza za Makundi yao, na Wiki hii, Jumanne na Jumatano, wanaingia Mechi Dei 2 huku baadhi zikiwa tayari zimejijengea nafasi nzuri.
Katika Mechi Dei 2 zipo Mechi tatu hivi zenye mvuto kwa kuwa na ushindani na nazo ni ile ya SL Benfica v FC Barcelona na zile mbili za ‘Kundi la Kifo’ za -AFC Ajax v Real Madrid CF na Manchester City FC v Borussia Dortmund.
ZIFUATAZO ni DONDOO FUPI FUPI KUHUSU MECHI HIZO:
MECHI za JUMANNE=Oktoba 2
KUNDI E
-FC Nordsjælland v Chelsea FC
Juventus v FC Shakhtar Donetsk
>> Chelsea washawahi kumaliza kama Washindi wa Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 7 kati ya 9 walizoshiriki na katika hizo mbili ambazo hawakuwa Washindi pia walifanikiwa kusonga Raundi inayofuata.
>> Shakhtar wameweza kuifunga Klabu ya Italy kwenye mara yao ya mwisho kucheza Mechi Nchini humo kwa kuichapa AS Roma bao 3-2 kwenye Msimu wa 2010/11 wa UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Rundi ya Mtoano ya Timu 16.
KUNDI F
-FC BATE Borisov v FC Bayern Munich
-Valencia CF v LOSC Lille
>> Bayern, waliowahi kuwa Mabingwa wa Ulaya mara 4, wamefungwa Mechi 3 kati ya 4 walizocheza mwisho ugenini kwenye Mashindao haya.
>> Valencia hawajawahi kufungwa na Klabu ya Ufaransa. Gemu 7 zimeleta ushindi mara 7 huku wakifunga Goli 18 na kufungwa 3 tu.

KUNDI G
-SL Benfica v FC Barcelona
-FC Spartak Moskva v Celtic FC
>> Siku zote Klabu hizi zikikutana kwenye Mashindano haya Mshindi wake hufika Fainali na kutwaa Kombe na hii ilianza kwa Benfica Mwaka 1961.
>> Celtic watataka mafanikio kwenye rekodi yao ya kucheza ugenini kwenye michuano hii ambayo tangu Msimu wa 2001/2 wamefungwa Mechi 19 kati ya 20 za ugenini isipokuwa hiyo moja waliyotoka sare ya 1-1 na Barcelona Mwezi Novemba 2004 huko Nou Camp.
KUNDI H
-Galatasaray AÅž v SC Braga
-CFR 1907 Cluj v Manchester United FC
>> Galatasaray wanainga kweye Mechi hii wakiwa wamefungwa mara moja kati ya 9 walizocheza Mashindano ya Klabu za Ulaya.
>> Man United, Msimu uliopita, walishinda mara moja tu ugenini kwenye michuano hii walipoifunga Galatei ya Romania bao 2-0 kwa bao za Wayne Rooney.
MECHI za JUMATANO=Oktoba 3
KUNDI A
-FC Porto v Paris Saint-Germain FC
-FC Dynamo Kyiv v GNK Dinamo Zagreb
>> Mara nyingi Klabu za Ufaransa hazifanyi vizuri nyumbani kwa Porto na ni FC Nantes pekee iliyoshinda 2-0 Mwaka 1971/72 kwenye UEFA Cup na mara nyingine zote 8 Porto imeshinda 6 na sare 2.
>> Zagreb wameshafungwa Mechi 7 mfululizo hadi sasa kwenye Mechi za Makundi za michuano hii.
KUNDI B
-Arsenal FC v Olympiacos FC
-FC Schalke 04 v Montpellier
>> Arsenal na Olympiacos pia zilikutana kwenye Mechi Dei 2 Msimu uliopita na Arsenal walishinda 2-1 huku Alex Oxlade-Chamberlain akifunga bao la kwanza katika Mechi yake ya kwanza ya michuano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na bao la pili kupigwa na Santos.
>> Schalke wameshinda Mechi zao zote 3 dhidi ya wapinzani kutoka Ufaransa.
KUNDI C
-RSC Anderlecht v Málaga CF
-FC Zenit St Petersburg v AC Milan
>> Anderlecht wameshinda Mechi 7 na kutoka sare mbili katika Mechi zao 9 walizocheza nyumbani kwenye Mashindano haya.
>> Zenit wanasaka kuendekeza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 16 za nyumbani za Mashindano ya UEFA rekodi ambayo imeendelea tangu wafungwe na Real Madrid Mwaka 2008 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
KUNDI D
-AFC Ajax v Real Madrid CF
Manchester City FC v Borussia Dortmund
>> Ajax, kwenye Msimu wa 2011/12, walifungwa 3-0 na Real Madrid wakiwa nyumbani na hivyo kushindwa kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya michuano hii.
>> Klabu za Man City na Borussia Dortmund hazijawahi kukutana kwenye Mechi za Ulaya.












































About Author

Advertisement

 
Top